Friday, October 19, 2012

WINGU LA VURUGU ZA KIDINI LAENDELEA KUTANDA TANZANIA

TANZANIA,
Vurugu zinazohusishwa na dini zimeendelea nchini zikisababisha  kuuawa kwa askari polisi mmoja kisiwani Zanzibar, maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoa tamko zito, pamoja nakupandishwa kizimbani kwa Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda (54) na wenzake 49 pamoja na tukio la Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kususia kikao. 

Askari aliyeuawa ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia huko Zanzibar Koplo Said Abdulrahman, ambaye ameuawa kwa kupigwa mapanga na wafuasi wanaodaiwa ni wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (Jumiki) katika vurugu zinazoendelea mjini Zanzibar baada ya kiongozi wa kikundi cha uamsho sheikh Farid kupotea na kuibuka hisia za kushikiliwa na jeshi la polisi kwa siri.

kwa mujibu wa Jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema wafuasi wa Uamsho walimvamia askari huyo majira ya saa 6:30 siku ya jumatano eneo la Bububu ambapo walimshambulia na kuichoma piki piki aliyokuwa anaitumia


kwa mujibu wa jeshi lapolisi kisiwani humo watu 10 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho pamoja na vurugu.


Wakati huohuo,kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar lilivamiwa na wafuasi wanaoaminika kuwa ni wa kundi la Uamsho na kusababisha uharibifu wa mali ikiwamo kuvunjwa vioo na madirisha kung’olewa.

kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Masoud, alisema wafuasi wa Uamsho walilivamia kanisa hilo na kulishambulia kwa mawe.

No comments:

Post a Comment