Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Sunday, April 6, 2014

Hali ya Michael Shumacher yaimarika

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/04/140404122707_michael_schumacher_304x171_getty_nocredit.jpg 
Bingwa wa zamani wa mbio za magari ya langalanga ya F1, Michael Schumacher ameanza kuonyesha hali ya kupata fahamu baada ya miezi kadha ya kuwa katika hali ya kutojitambua.
Wakala wake Sabine Kehm amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema Schumacher "anaendelea vizuri", akisema kwamba wana "uhakika"wa kupona kwake.
Madaktari nchini Ufaransa wanafanya jitihada za kumwondoa katika hali ya kutojitambua, bingwa huyo mara saba wa F1.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45-alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya ajali wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa Desemba 29,2013.
"Tuko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake, sisi na timu nzima ya madaktari na wauguzi wa hospitali ya Grenoble," amesema Bi Kehm.

Monday, March 10, 2014

Orodha ya Wanasoka 10 tajiri duniani, etoo' no.3.

Ni miongoni mwa zile stori ambazo mashabiki wengi hupenda kuzifahamu au hata kuziongelea kwenye vijiwe mbalimbali lakini uhakika umetolewa na mtandao unaodili na stori za soka kwa sana.
Katika listi hiyo iliyotajwa leo, Ronaldo amemrithi David Beckham ambaye alistaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita ambapo Ronaldo ana utajiri wa paundi millioni 122.
Lionel Messi ameshika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa paundi millioni 120, nafasi ya tatu imekamatwa na muafrika pekee kwenye listi hii ambae ni Samuel Etoo mwenye utajiri wa paundi millioni 70, Rooney anafatia kwa utajiri wa paundi millioni 69 huku Kaka akishika nafasi ya 5 kwa utajiri wa paundi millioni 67.
Listi inaendelea kama ifuatavyo
players copy

Chanzo:millardayo.com













Saturday, March 8, 2014

CHELSEA WASHINDA 4-0 DEMBA BA APIGA 2.

View image on Twitter 
Timu ya Chelsea imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuwatungua Totenham kwa mabao 4-0, mabao yakifungwa na Etoo dk.56, Hazard dk  60, Demba Ba dk.88 & 90.


Referee: Michael Oliver
Lineups
Chelsea: Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Ramires, Matic, Lampard; Schurrle, Hazard; Eto'o/Demba Ba.

Tottenham Hotspur: Lloris; Naughton, Dawson, Kaboul, Vertonghen; Bentaleb, Sandro; Walker, Lennon, Sigurdsson; Adebayor

Tuesday, March 4, 2014

Luis Suarez asaini mkataba mpya


 
Everton ikiwa mbele ya Chelsea, katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza, baada ya kuifunga Swansea mabao (2-1), na kuipa shinikizo the Bleus ambayo itakwaruzana na Arsenal leo jumatatu. Tottehnam imefungwa na Southampton mabao (3-2).
Chelsea ambayo ilishapoteza mara moja msimu huu, imekua na shauku toka tarehe 5 mwezi oktoba kusogea mbele ikitoka kwenye nafasi ya 4. Chelsea ina alama 34, ikiwa mbele ya Arsenal alama 1.
Liverpool kwa sasa ndio inaongoza.



Hata hivo, Mshambuliaji mahiri wa Klabu ya Liverpoool Luis Suarez amesaini mkataba kuendelea kusakata gozi kwenye Klabu hiyo ya Liverpool.

Awali mkataba wa Suarez ambaye alijiunga na klabu hiyo January 2011 na akiwa tayari amekwishafunga mabao 17 msimu huu, ulitaraji kukamilika mwaka 2016.

Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 26, amesema amefurahi kufikia makubaliano ya kuendelea kuitumikia kwa muda mrefu klabu hii ya Liverpool, akibaini kwamba timu hio ina wachezaji mahiri, na inazidi kuimarika kila wakati.

Naye kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa hiyo ni habari njema kwa kila mdau wa Klabu ya Liverpool, wakiwemo wamiliki wa klabu lakini muhimu Zaidi Mashabiki wa klabu hiyo.

“Suarez ni mchezaji wa kiwango cha dunia, mwenye kipaji cha hali ya juu, na kwa kuendelea kuwa naye wakati huu ni jambo la msingi katika kile tunacholenga kukipata hapa klabuni kwetu”, amesema Brendan.

Kocha huyo wa Liverpool amesema wtaendelea kushuhudia ubora wa Luis Suarez siku zijazo,akiwa ndani ya jezi za Liverpool.

Kesi ya mauaji ya bingwa wa mbio za paralympic Oscar Pistorus inaendelea

Оскар Писториус в зале суда в Претории 03/03/2014

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mwenye ulemavu wa Miguu Oscar Pistorius raia wa Afrika Kusini, hii leo imeingia siku yake ya pili kwa upande wa utetezi kuwahoji mashahidi wa Serikali.

Hii leo shahidi wa pili kwenye kesi hiyo ambaye ni jirani wa Oscar Pistorius ameieleza mahakama namna alivyosikia milio ya risasi na kelele za kuomba msaada toka kwa mpenzi wa Pistorius na kwamba jambo hilo lilimfanya ahisi kulikuwa na ujambazi kwa jirani yake.
Lakini wakati shahidi huyu wapili akieleza kile alichokisikia, hapo jana shahidi wa kwanza kwenye kesi hiyo alijikuta matatani wakati akihojiwa na upande wa utetezi kutokana na kutofautiana kwa kauli zake na hata wakati fulani kuangua kilio kilichopuuzwa na mawakili wa Pistorius.
Katika hatua nyingine jaji anayesikiliza kesi hiyo, Thokozile Masipa amevionya vyombo vya habari dhidi ya kuchapisha picha za mashahidi ambao wamekataa sura zao kuoneshwa hadharani na kwamba atavichukulia hatua vyomb vyote vya habari vitakavyokiuka amri ya mahakama.
Hapo jana kituo kimoja cha televisheni nchini humo kilionesha picha ya shahidi ambaye ni mhadhiri wa chuo kimoja mjini Pretoria wakati akihojiwa na upande wa utetezi hali iliyoamsha toka kwa wanaharakati.

Sunday, March 2, 2014

Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu

CFC_910be.jpgTimu ya Chelsea imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuicharaza Fulham magoli 3-1 na kujikusanyia pointi 63.
Mabao yote matatu ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji wake Andre Schurrle akiyafunga katika dakika ya 52, 65 na 68, huku bao la kufutia machozi la Fulhamlikifungwa na Heitinga katika dakika ya 74.

Arsenal iliyokuwa ikifukuzana na Chelsea kwa tofauti ya pointi moja imejikuta ikiachwa pointi nne zaidi baada ya kucharazwa na Stoke goli 1-0. Arsenal imebaki na pointi 59 na kuporomoka hadi nafasi ya tatu, huku Liverpool ikipanda, nayo ikiwa na pointi 59 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga.
Wakati Newcastle ikiididimiza Hull kwa mabao 4-1, nayo Everton iliibanjuaWest Ham bao1-0.
Msimamo wa ligi kuu ya England baada ya michezo hiyo ya Jumamosi, Chelsea inaongoza kwa pointi 63 baada ya kucheza michezo 28 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 59 na Arsenal ni ya tatu ikiwa pia na pointi 59.
Mancity ni ya nne ikiwa na pointi 57 lakini ikiwa imecheza michezo 26 tu, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda kileleni iwapo itashinda mechi zake mbili.
Manchester United mabingwa watetezi, iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 45 lakini imecheza michezo 27.
Mkiani kabisa ni Fulham yenye pointi 21 na mbele yake ni Cardiff yenye pointi 22.
Chanzo, bbcswahili (R.M)

Sunday, February 9, 2014

Serena akacha Indian Wells

 
HESABU za waaandaaji wa michuano ya tenisi ya Indian Wells BNP Paribas Open kuona nyota namba moja kwa wanawake, Serena Williams, anashiriki kipute cha mwaka huu zimeyeyuka.
Serena ambaye mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ni miaka 13 iliyopita, alisema juzi kuwa hatashiriki baada ya kutafakari kwa kina ushiriki wake.
“Baada ya kutafakari kwa kina, sitaweza kushiriki michuano ya Indian Wells BNP Paribas Open kwa mwaka huu,” alisema nyota huyo huku akiwatakia kila la heri washiriki katika michuano hiyo inayotarajiwa kuwaleta pamoja nyota mahiri wake kwa waume.
Akizungumzia uamuzi wa Serena, Mkurugenzi wa michuano hiyo, Steve Simon, alisema wanamkaribisha katika michuano ya mwaka ujao.

Saturday, February 8, 2014

MALINZI: TUNA MZIGO WA MADENI KUTOKA KWA TENGA

 

 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema changamoto kubwa linaloikabili sasa ni madeni ya mamilioni ya fedha waliyoyarithi kutoka uongozi uliopita wa Rais, Leodegar Tenga.


Akizungumza  katika tathimini yake ya siku 100 tangu alipochaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alisema madeni hayo ni makubwa ukilinganisha na kipato cha TFF kinachotegemea zaidi mapato ya milangoni ya mechi mbalimbali.



"Madeni tuliyoyakuta ni makubwa, lakini mengine tumegundua ni hewa, hivyo yanafanyiwa uhakiki ili tujue madeni halisi ili tuweze kuyalipa," alisema Malinzi aliyeingia madarakani Oktoba 27, mwaka jana.

"Pia tunafanya mazungumzo na watu wanaoidai TFF ili watupe masharti nafuu ya kulipa madeni hayo."

Kauli ya Malinzi imekuja ikiwa imepita miezi sita tangu TFF ipate aibu ya mabasi yake kukamatwa na Kampuni ya Udalali ya Flamingo ili kufidia deni la zaidi ya Sh50 milioni.


Chanzo:Mwananchi mtandaoni