Friday, March 30, 2012

ECOWAS WAHAIRISHA MKUTANO WA MALI.

Wawakilishi wa Umoja wa Kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wamehairisha mkutano wao na viongozi wa seriali ya uasi ya Mali uliokuwa ufanyike nchini humo na sasa watakutana Mjini Abidjan Ivory Coast.Kwa Mujibu wa Taarifa za Ikulu kutoka nchini Ivory Coast hali ya usalama nchini Mali yakiwemo maandamano ya Kuunga mkono mapinduzi ni moja ya sababu za Kuhamishwa Mkutano huo.
Imeripotiwa kuwepo kwa maandamano makubwa katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako na  uwanja wa ndege nchini Mali katika eneo la kupaa na kutua hali inayofanya usafiri kuwa mgumu kwa njia ya anga nchini humo.
Siku ya Jumatano maelfu ya wananchi wa Mali waliandamana kupinga kuingiliwa na nchi za kigeni huku wakiyaunga mkono maandamano hayo.
Waasi nchini humo waliipindua serikali ya rais Toure kwa kile walichokiita kushindwa kushughulikia suala la waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi hiyo ambapo tayari viongozi hao wa mapinduzi wametangaza kuwepo kwa katiba mpya huku sehemu kubwa ya vifungu katika katiba ya zamani vikiwemo ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza na kutembea,pia  wametangaza kuwepo kwa uchaguzi ingawa waliohusika katika mapinduzi awataruhusiwa kushiriki uchaguzi huo.
Wakati huo huo nchi jirani na Mali zikiwemo Ivory Coast na ghana  zimetishia kufunga mipaka yao inayopakana na nchi hiyo kuanzia saa72 zijazo ikiwa majeshi ya waasi hayatakabidhi madaraka kwa wananchi.Pia nchi zote za ECOWAS zimesema zitaizuia mali kutumia bandari zao katika usafiridhaji. Kikwazo kingine ni kufungwa kwa akaunti ya serikali ya nchi hiyo katika benki ya Ukanda wa magharibi ya ECOWAS pia benki hiyo imezuiwa kutoa pesa kwa benki binafsi nchini Mali.

No comments:

Post a Comment