A
Picha na AFP
RIYADH_SAUD ARABIA,
Waziri wa mambo ya nje wa Mrekani Hillary Clinton leo amekutana na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Saud Arabia Prince Al-Faisal na yule wa Kuwait SheikhSabah Khaled huko Riyadh Saud Arabia katika muendelezo wa kujadili juhudi za kukomesha machafuko ya Syria.
Mkutano huo ni maandalizi ya mkutanowa nchi 60 zinazojiita "Marafiki wa Syria" utakaofanyika mjini Istanbul, Uturuki leo jumapili. Clinton pamoja na wanadiplomasia kutoka nchi nyingine zinazounga mkono makundi ya upinzani ya Syria wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo wa Istanbul.
Marekani hata hivyo bado inapinga Kuwapa silaha wapinzani wa Syria pendekezo kutoka kwa baadhi ya nchi za Ghuba huku ikisisitiz umuhimu wa kuyaunganisha makundi ya upinzani na kuhakikisha huduma za kibinadamu zinatolewa nchini Syria.
Mgogoro nchini Syria umefikia kipindi cha mwaka mmoja sasa huku juhudi za kimataifa zikishindwa na kutawaliwa na Upinzani kati ya nchi za Kiamgharibi dhidi ya urusi na China.
No comments:
Post a Comment