Sunday, April 22, 2012

MAJESHI YA SYRIA YAPAMBANA NA WAASI KARIBU NA DAMASCUS

SYRIA -Ikiwa ni miezi kumi tangu kuanza kwa maandamano ya kupingwa kwa utawala wa Rais Bashar Al-assad wa Syria mapigano yameripotiwa karibu na mji mkuu wa Damascus huku Douma tangu leo asubuhi. Imedaiwa waasi wamesogea mpaka eneo hilo wakielekea mji mkuu wa nchi hiyo huku gavana wa jimbo hilo akiongelea juhudi za kusitisha mapigano na kuzungumza  "Wengi tumezungumza nao na wameondoka natumaini wakirudi watarudi na njia nzuri" alisema gavana Hussein Makhloufa  alipokuwa akiongea na waangalizi kutoka Umoja wa nchi za kiarabu kabla hawajaingia katika mi mkuu wa nchi hiyo katika maeneo yenye vurugu.

             Jeshi la serikali tayari lipo eneo hilo na limeanza operesheni ya nyumba kwa nyumba kuwakamata watu linaowashuku kuhusika na uasi, ambapo waandishi wa habari walioneshwa silaha za Mabomu zilizotengenezwa kienyeji ambazo jeshi hilo limezikamata kutoka kwa wananchi.

Hata hivyo kikundi pinzani kinachoangalia haki za binadamu nchini Syria kimesema Serikali imewakamata watu 200 katika uvamizi huo wa Douma ambao ni moja ya miji yenye upinzani mkali kwa rais Al-assad.

Imedaiwa kikundi cha The Free Syrian Army (FSA) kimekamata baadhi ya maeneo ya Damascus, hallasta na Douma ingawa bado kinapata upinzani mkali kutoka kwa majeshi yenye silaha kali ya Serikali kama anavyokiri mmoja wa wapiganaji wa waasi kwa jina Abu Thaer. amabye anasema jeshi la nchi lina silaha kali ikiwamo ndege na magari ya kivita wakati wao wanabunduki aina ya Riffle, na mabomu madogo madogo.


Syria imekuwa katika machafuko kwa miezi kumi sasa ambapo wananchi wanomppinga rais wa nchi hiyo wanapambana na vikosi vya usalama kumtaka aondoke madarakani.


No comments:

Post a Comment