Timu ya Chelsea imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuicharaza Fulham magoli 3-1 na kujikusanyia pointi 63.
Mabao yote matatu ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji wake Andre Schurrle akiyafunga katika dakika ya 52, 65 na 68, huku bao la kufutia machozi la Fulhamlikifungwa na Heitinga katika dakika ya 74.
Arsenal iliyokuwa ikifukuzana na Chelsea kwa tofauti ya pointi moja imejikuta ikiachwa pointi nne zaidi baada ya kucharazwa na Stoke goli 1-0. Arsenal imebaki na pointi 59 na kuporomoka hadi nafasi ya tatu, huku Liverpool ikipanda, nayo ikiwa na pointi 59 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga.
Wakati Newcastle ikiididimiza Hull kwa mabao 4-1, nayo Everton iliibanjuaWest Ham bao1-0.
Msimamo wa ligi kuu ya England baada ya michezo hiyo ya Jumamosi, Chelsea inaongoza kwa pointi 63 baada ya kucheza michezo 28 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 59 na Arsenal ni ya tatu ikiwa pia na pointi 59.
Mancity ni ya nne ikiwa na pointi 57 lakini ikiwa imecheza michezo 26 tu, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda kileleni iwapo itashinda mechi zake mbili.
Manchester United mabingwa watetezi, iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 45 lakini imecheza michezo 27.
Mkiani kabisa ni Fulham yenye pointi 21 na mbele yake ni Cardiff yenye pointi 22.
Chanzo, bbcswahili (R.M)
No comments:
Post a Comment