Friday, March 14, 2014

SITTA:KURA YA SIRI

 

Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amezungumzia uwezekano wa kutumia kura ya siri katika kuamua ibara nyeti katika Rasimu ya Katiba. Sitta aliyechaguliwa juzi kushika wadhifa huo, alisema atashirikiana na kamati ya uongozi itakayoundwa ya wenyeviti wa Kamati 15 za Bunge hilo na kamati ya ushauriano kupata jawabu la suala hilo. - See more at: http://bungelakatiba.blogspot.com/2014/03/samuel-sitta-kura-ya-siri.html#sthash.XysswCrd.dpuf Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, Sitta alisema: “Unajua kuna baadhi ya vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba ni vizuri vipigiwe kura ya wazi na vingine ambavyo ni nyeti zaidi vipigiwe kura ya siri.” Alisema si vizuri vifungu vyote vipigiwe kura sawa, yaani si lazima zote ziwe za siri au ziwe za wazi. Alitoa mfano wa ibara inayosema kutakuwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na kusema: “Hatuwezi kushindana katika suala la kuwapo kwa Mahakama na ni wazi kuwa jambo hilo mnaweza kupiga kura ya wazi. Nasema hivyo kwa sababu Katiba yoyote lazima ionyeshe mihimili yote ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama.” Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alishinda kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika juzi kwa kura 487 kati ya 563 (sawa na asilimia 85). Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye kaulimbiu yake ni ‘kasi na viwango’, alisema vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba vinavyoweka misingi ya Katiba, ni vizuri vikapigiwa kura ya siri. - See more at: http://bungelakatiba.blogspot.com/2014/03/samuel-sitta-kura-ya-siri.html#sthash.XysswCrd.dpuf

No comments:

Post a Comment