Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.
"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.
No comments:
Post a Comment