Takribani miaka 17 tangu baba wa taifa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere aionye Tanzania juu ya ubaguzi, 'maono' yake yameanza kutimia baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vinavyowataka wananchi wenye asili ya Pemba kuondoka Unguja siku chache baada ya Jumuiya ya Uamsho Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) kuukataa muungano wa Tanzania na kutaka Zanzibar ijitenge na Tanzania bara(Zamani Tanganyika). Vipeperushi hivyo vinavyosambaza na kundi lililojitambulisha kama 'Watu wa Unguja' limetoa tahadhari kwa watu wa Pemba kuondoka Unguja huku likiwatuumu kwa kuchochea vurugu na kuanyang'anya ardhi yao.
Kundi hilo pia katika vipeperushi hivyo limeushutumu Jumuiya ya Uamsho Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) kuwa ni kundi la kisiasa linalojitokeza kama kundi la dini.
“Watu wa Unguja tunatoa ujumbe mahususi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete…. Tumechoka kuishi na Wapemba katika kisiwa chetu cha Unguja, kwani ni watu wasio na fadhila ya aina yoyote ile,” isehemu ya kipeperushi hicho inasema na kuendelea;
“Hivyo, tunakuomba ufanye mazungumzo na Rais wa Zanzibar ili Wapemba wapewe kisiwa chao cha Pemba.”
Vipeperushi hivyo pia vimewatuhumu wapemba kuwa na asili ya Msumbiji na kutaka Pemba iondolewe katika Muungano na Tanganyika irudishwe na kufanya Muungano na Unguja kwani wanaochochea vurugu hizo ni watu kutoka Pemba. huku kikiwataja baadhi ya viongozi kwa majina.
No comments:
Post a Comment