Monday, June 11, 2012

WAZIRI SAITOTI NA NAIBU WAKE WAFARIKI KWA AJALI YA NDEGE KENYA.

Nairobi-Kenya,


Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya Profesa.George Saitoti na Naibu waziri wake Orwa Ojode na maafisa wengine sita(6)  wamefariki dunia baada ya kupata ajali na Helikopta ya Polisi huko Ngong karibu na Nairobi.

Imeeelezwa kuwa Saitoti na wenzake walikuwa wakielekea eneo la Sotik kwa ajili ya mkutano wa usalama. Saitoti ambaye alikuwa ni moja wa mawaziri wa Serikali ya rais Mwai Kibaki, aliwahi pia kuwa makamu wa rais kati ya mwaka 1976 na 1979 na alitangaza nia ya kugombea urais katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu akiwa ni moja ya wanasiasa wakongwe na wanaoheshimika nchini humo.
 Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema  waliiona helikopta hiyo ikiyumba kabla ya kuanguka na kushika moto, ambapo watu wa Msalaba mwekundu wamesema miili ya marehemu hao imeungua vibaya kiasi cha kutotambulika. Baada ya ajali hiyo polisi walilizingira eneo hilo na mmoja wa makasmishna alihidi kuwa Wangetoa taarifa kamili baadaye.

Saitoti atakumbukwa kwa kuiongoza Kenya katika vita dhidi ya kundi la Kigaidi la Al Shabaab la Somalia, kupinga rushwa na ubaguzi wa kidini na kikabila ambapo mara kadhaa aliwasihi Wakenya kutomchagua mtu kwa msingi wa rushwa , dini au Ukabila.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki ametoa taarifa yake ambapo amesema vifo hivyo ni msiba mkubwa kwa taifa, ambapo kwa niaba ya serikali na watu wa Kenya ametuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na ndugu wa marehemu. Rais Kibaki  amesema Saitoti atakumbukwa milele kutokana na uchapaji kazi wake na kujitolea muda wake wote katika kuhudumia watu wa Kenya.
ANGA ZA KIMATAIFA Inaungana na Familia za marehemu na Wananchi wote wa Kenya kuomboleza kipindi hiki kigumu, Mwenyezi Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali Pema Peponi, AMEN.

No comments:

Post a Comment