Ufaransa na Uingereza leo wanakutana uso kwa uso katika mihuano ya mataifa ya Ulaya(EURO 2012) huko Donetsk.
Ufaransa almaarufu 'Les Bleus' wanaingia dimbani leo wakiwa na rekodi ya kuishinda mara mbili Uingereza hapo Mwaka 1984 na Mwaka 2000.
Kwa Ujumla timu hizo zimekutana mara 30 , Uingereza ikashinda mara 16, kupoteza mara 6 na kutoka sare mara 6, ingawa Ufaransa ina rekodi ya kwa Uingereza katika michuano hiyo.
Kwa upande wao Ufaransa ambao wataongozwa na nyota Karim Benzema wanamajeruhi Blaise Matuidi na Yann M’Vila ambao licha yakurudi mazoezini haijafahamika kama watakuwa safi kucheza mchezo wa leo.
Ufaransa (4-2-3-1): Lloris; Debuchy, Rami, Mexes, Evra; M'Vila, Cabaye; Ribery, Nasri, Malouda; Benzema.
Uingereza (4-4-1-1): Hart; Johnson, Terry, Lescott, Cole; Milner, Gerrard, Parker, Downing; Young; Welbeck.
No comments:
Post a Comment