Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars imeondoka hapo janakuelekea Abdjan Ivory coast kwa mchezo wake wa kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2014 nchini Brazil dhidi ya Ivory Coast huku ikiwaacha Kiungo Haruna Moshi 'Boban' na beki, Nassor Masoud waliomajeruhi na hivyo kufikisha jumla ya majeruhi wanne walioachwa baada ya Thomas Ulimwengu na kiungo, Nurdin Bakari.
Katibu Mkuu wa shirikisho la soka la Tanzania Anjetile Osiah aliwaamia waandishi wa habari kuwa wachezaji hao wamebakizwa kutokana na kuwa wagonjwa.
Hata hivyo timu hiyo ililazimika kusota kwa muda wa masaa matano katika Uwanja wa Jomo Kenyata nchini Kenya baada ya ndege waliotarajia kusafiri nyao kubadilishwa na hivyo kufika Ivory coast mishale ya saa 3:00 usiku badala ya mcahana kama walivyotarajiwa, ingawa kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen alisema hali hiyo haitaathiri timu yake amayo imeshajiandaa vizuri kutoka nyumb
Mara baada ya mechi hiyo Taifa Stars itarejea nchiniJuni 5 na kwa maandalizi ya kuikabili Gambia ambayo itakuwa mgeni wao Juni 10 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kila la Kheri Taifa Stars katika kuipeperusha bendera ya Taifa Letu!
No comments:
Post a Comment