hatimayeserikali ya Syria imesalimu amri na kuyaruhusu mashirika ya kutoa misaada kuanza shughuli zao katika mikoa minne ya Homs, Idlib, Deraa na Deir al-Zour iliyopatwa na mapigano makubwa kati ya majeshi ya Serikali na Waasi.
Kwa mujibu wa Umoja Wa mataifa serikali ya Syria imekubali kuyaruhusu mashirika ya kutoa misaada kufanya kazi katika mikoa hiyo. Afisa mmoja wa Umoja huo amesema kuwa serikali ya Syria imekubali kwa maandishi kuwaachia wafanya kazi wa kutoa misaada pamoja na magari yenye vyakula na misaaada mingine kuingia. ndani ya mikoa hiyo.Afisa huyo alisema kuwa suala hilo litakuwa ni kipimo kikubwa cha Syria kwa jumuiya ya kimataifa kama ina nia nzuri na wananchi wake.
No comments:
Post a Comment