Aliyewahi kuwa bingwa mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon na bingwa mara saba wa Grand Slam, Mmarekani Venus Williams, ameondolewa katika siku ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza, baada ya kufungwa na mchezaji kutoka Urusi, Elena Vesnina ambaye yupo nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis kwa upande wa wanawake.
Venus, ambaye anaugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome, alishindwa kwa seti 6-1 6-3 . nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni.
Hata hivyo Serena alisema hawezi kukata tamaa na kustaafu, "Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alisema Serena.
"Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu."
Mara ya kwanza Williams kushindwa katika raundi ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1997, wakati ambao ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo na hakuwa miongoni mwa wachezaji bora wa tennis.
Serena amekumbwa na mkosi katika mashindano hayo ambapo tangu mwaka2008, hajawahi kuibuka bingwa katika mashindano hayo.
Serena ameonekana kushuka kiwango tangu alipoanza kuugua ugonjwa huo ambao unamfanya ajisikie mchovu na kusumbuliwa na maumivu katika viungo vya mifupa yake.
No comments:
Post a Comment