Sunday, February 17, 2013

Padri wa Kikatoliki auawa Zanzibar .

ZANZIBAR-TANZANIA,
http://t1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSw2QWBbKKfbw96OHur67PO3KyNw1YdzT2FkzGMyQJMOzOVbzp6P_05nQWatu waliokuwa na bunduki leo wamempiga risasi na kumuuwa Kasisi wa katoliki Bw. Evarist Mushi ambaye ni Paroko wa Parokia ya Minara Miwili – Zanzibar likiwa ni shambulizi la pili kuwahi kufanywa katika miezi ya karibuni katika kisiwa hicho ambacho idadi kubwa ya wakaazi wake ni Waislamu. Msemaji wa polisi kisiwani humo Mohammed Mhina amesema  alizuiwa na vijana wawili nje ya  lango la kanisa , kabla ya mmoja wao kumpiga risasi kichwani.

 Mhina amesema kwa sasa kiini cha shambulizi hilo hakijajulikana, lakini polisi inafanya msako wa kuwanasa majambazi hao. Mnamo siku ya Krismasi, watu waliokuwa na bunduki  walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya kasisi wa kikatoliki wakati akirejea nyumbani kutoka kanisani. 

Haijabainika kama mashambulizi hayo mawili yanahusiana, au  ikiwa yamechochewa na hisia za kidini. Mwezi Novemba mwaka jana, washambuliaji walimmwagia kemikali usoni na kifuani mhubiri mmoja wa kiislamu, na kumekuwa na hofu baina ya jamii hizo mbili kisiwani Unguja.

No comments:

Post a Comment