Thursday, May 2, 2013

WAASI WA M23 WAISOGELEA KAMBI YA MONUSO HUKO DRC


Baadhi ya askari wa kundi la M2

RUTSHURU-DRC,Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Monusco umesema kuwa waasi wa Kundi la M23 wamesogeza mbele Ngome yao kwenye mita 30 karibu na makao makuu yao Huko Kiwanja mtaani Rutshuru.

Katika hatua nyingine msemaji wa Monusco Felix Prosper Bass anasema zaidi ya wapiganaji 65 kutoka kundi hilo la M23 wamejisalimisha na hivyo kupokelewa kwenye Tume hiyo na kwamba hilo linaweza kuwa ndiyo sababu ya wao kusogeza ngome yao.
Kwa upande wake kiongozi wa Kundi la M23, Betrand Bisimwa amesema kuwa Hizo ni propaganda za serikali ya Kinshasa ikiwa imeshirikiana na Monusco katika kudhihirisha nia yao ya kutaka kuanza mapigano.
Nayo Mashirika ya Kiraia katika Jimbo la Kivu ya kaskazini kupitia naibu mwenyekiti na msemaji wa mashirika hayo, Omari Kavota pia yamethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa kundi hilo la M23 limeweka vizuizi katika maeneo kadhaa huko mashariki mwa Kongo.
Hatua iliyochukuliwa na kundi la M23 inaelezwa kuongeza wasiwasi miongoni mwa raia huko Mashariki mwa DRC pamoja na kuzorota kwa hali ya amani.
Hayo yanatokea wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea na maandalizi ya kupeleka kikosi maalum cha kimataifa kitakachojumuisha wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment