Saturday, April 5, 2014

PICHA YA RAIS OBAMA YAWATOKEA PUANI SAMSUNG.

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/04/140404090825_obama_picha_512x288_bbc_nocredit.jpg 

Ikulu ya Whitehouse imeikashifu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu nchini Marekani David Ortiz kama tangazo la kibiashara.
Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki.
Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia kwa mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.
Bwana Carney amesema kuwa mawakili wa White House wanashauriwa kuhusu kitendo hicho cha Samsung.
"bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,'' alisema Carney
Ortiz alimpa Rais Obama Jezzi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na jkisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama 'Selfie'.
"Nilimpa Jezzi na wapiga picha waka wanatupiga picha, basi nilijhisi na mimi kujipiga naye picha'' alisema mchezaji huyo.
Alikana kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa kwa picha hio.

Friday, April 4, 2014

Vikosi vya Marekani vyawasili Uganda kumsaka Kony

http://www.dw.de/image/0,,6478206_10,00.jpg

Kampala. Vikosi vya Marekani kwa ajili ya kumkabili kiongozi wa kundi la Lord Resistance Army (LRA) Joseph Kony vimewasili nchini Uganda huku vikiwa na vifaa vya kisasa zikiwamo ndege zenye uwezo wa kujaza mafuta angani.
Taarifa zimesema kuwa askari hao 150 waliwasili siku tatu zilizopita na kwamba sasa wanatazamiwa kuanzisha msako mkali katika maeneo ya mpakani mwa Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako kiongozi huyo anaaminika kujifisha.
Hivi karibuni Rais Barack Obama aliidhinisha kutumwa kwa vikosi hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na Umoja wa Afrika za kumsaka Kony ambaye pia anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu(ICC) kutokana na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Askari hao wamewasili wakiwa na vifaa vya kisasa ikiwamo ndege aina ya CV-200 yenye uwezo wa kujaza mafuta ikiwa angani na kwamba mkakati wao wa kwanza ni kuelekea kwenye misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ofisa habari katika ubalozi wa Marekani nchini Uganda Daniel Travis alithibitisha kuwasili kwa askari hao lakini hata hivyo hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi.
“Hatuwezi kueleza zaidi kuhusiana mahali ambako vikosi hivyo vipo zaidi ya kusema kwamba vitakuwepo nchini kwa muda maalumu na hatutarajia kuona vinakuwepo zaidi ya muda ulioamuliwa,”alisema.
Vikosi hivyo vya Marekani vinatazamiwa kuongeza nguvu juhudi za kumsaka kiongozi huyo ambaye anatuhumiwa pia kwa kuwaandikisha askari watoto na kuhusika katika vitendo vya ubakaji.
Kwa muda mrefu vikosi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikiendesha msako dhidi ya Kony bila mafanikio yoyote kutokana na kuhamisha mara kwa mara maficho yake. Vikosi hivyo vya Afrika vinaundwa na askari kutoka Uganda, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

CHANZO:MWANANCHI

UZEMBE HATI YA MUUNGANO: SAINI ZA NYERERE,MSEKWA ZACHEZEWA

 
Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amekiri “kuchezewa” kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa. Alisema katika saini ya Nyerere kumeongezwa herufi “us” kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno “Msekwa” kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa. “Wale vijana walipoona document (nyaraka) haisomeki waliongeza “us” mwisho kwa kompyuta kwenye saini ya Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo hivyo lakini kibaki na maana yake,” alisema. Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya sheria hiyo ipo sawa ukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo. Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta “Msekwa”. “Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa chamber kwa AG waliongeza neno “Msekwa” kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100 hata mtu aje kuisoma kwa darubini,” alisema. Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume. Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti na madai ya Sitta. Sheria iliyopitishwa Z’bar Sitta alisema ili kuondoa utata, ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume (Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo, hakukuwa na Bunge. “Karume alitumia Baraza la Mapinduzi akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar,” alisema Sitta.