DAMASCUS,SYRIA- Majeshi ya serikali yamefanikiwa kutwaa baadhi ya vitongoji vitongoji vya mji wa Damascus kutoka kwa waasi wa kundi la Free Syrian Forces hapo jana baada ya mapigano yaliyodumu kwa muda wa siku mbili na kushuhudia mauaji ya Jumla ya watu 66 wakiwemo raia 26.
" Majeshi ya waasi yameondoka katika mji na majeshi ya serikali yameuchukua tena na kuanza operesheni ya kukamata watu nyumba kwa nyumba" alisema Mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la Kamal kutoka Ghouta huko Damascus.
.
Muongeaji wa kikundi cha waasi cha FSA, Mahel al-Naimi pia amethibitisha habari hizo na kusema majeshi ya Syria yameingia na kuchukua vitongoji hivyo ingawa wao bado wapo karibu na mji huo.
Wanaharakati walisema kiasi cha Vifaru 50 na magari mengine ya kivita yaliingia katika vitongoji hivyo hapo jana ambapo raia 19 na waasi waliuawa. Mmoja wa mashuhuda mjini humo Bw. Kfar Batna aliita vita hiyo kuwa "Vita ya mjini" na kueleza kuwa Miili mingi ya watu waliokufa imetapakaa katika mitaa ya mji huo.
Waasi hao walikua wameshikilia baadhi ya vitongoji vilivyo umbali wa kilometa 8 kutoka kati kati ya Mji mkuu wa Damascus.
Mfululizo wa vitendo vya umwagaji damu na vurugu mjini Syria vinazidi kuongezeka hali ilyowafanya waangalizi wa Umoja wa nchi za kiarabu kuondoka nchini humo ambapo umoja huo ambao unataka rais Al Asad ajiuzuru umepanga kufanya mkutano wake Februari 5 kujadili hatima ya Nchi hiyo.Umoja wa mataifa Pia umekuwa katika juhudi za kumaliza machafuko hayo ingawa wanchama wake China na Russia wenye Kura za Veto wameonekana kulega kuunga mkono azimio la kuchukuliwa hatua dhidi ya Serikali ya Syria.
No comments:
Post a Comment