Wednesday, February 1, 2012

MITT ROMNEY ASHINDA FLORIDA.

 
FLORIDA, MAREKANI,
Gavana wa zamani wa Massachusetts  Mitt Romney  amepata ushindi katika kinyang'anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kupitia chama cha Republican katika Jimbo la Florida siku ya Jumanne. Ushindi huo umemfanya Romney kuwa kinara wa kinyang'anyiro hicho akiwatupa wapinzani wake wa karibu  Bw.Gingrich na Bw.Santorum.
Matokea ya kinyang'anyiro katika Jimbo hilo yameonesha Romney amejipatia  47%  , Gingrich  32%, Santorum 13% na Paul akiambulia 7% ya kura zote.

Katika hotuba yake ya Ushindi Bw. Romney amepinga wazo kuwa kinyang;anyiro hicho kinakidhoofisha chama cha Republican :
"Kinyang'anyiro hicho  hakitugawanyi bali kinatuandaa" alisema bw.Romney akiwa Tampa Florida.

Mgombea huyo badala yake aligeuza kibao kutoka kwa wagombea wenzake kwenda kwa rais Obama  akisema rais huyo alichaguliwa kuongoza lakini amechagua kuongozwa kwa hiyo atoke nje ya njia kuwapisha wengine akitumia msemo wa manafilosofia maarufu  Thomas paine aliyesema"Ongoza,Ongozwa au toka kabisa kwenye Njia"
Kwa matokeo hayo Romney ameshika nafasi ya kwanza,akifuatiwa na  Gingrich alimaliza wa pili, huku Rick santorum akichukua nafasi ya tatu na Ron Paul ya nne.
Kwa upande wake Gingrich amesema maatokeo hayo yameongeza ushindani wa mwakilishi wa chama chao katika Uchaguzi ujao na akasisitiza kuendelea na kinyang;anyiro hicho.
"Tutaendelea kushindana kila sehemu na tutashinda na kurudi hapa Tampa kama wagombea wa Urais hapo mwezi wa nane" aliongea Gingrich kutoka aliongea makao yake  makuu huko Orlando. Gingrich aliongeza kuwa ataonesha ni kwa jinsi gani "nguvu ya umma" itashinda "Fedha" katika kinyang'anyiro hicho.

Mgombea mwingine aliyeshika nafasi ya tau Bwana Santorum amesema ataendelea kupambana na kuwataka wagombea wenzake kujikita zaidi katika hoja muhimu badala ya kupakana matope.

kwa upande wake Paul pia amejipa moyo wa kuendelea ambapo katika hotuba yake aliyoitoa huko Nevada baada ya kumpigia simu Romney na kumpongeza alisema "Nimemwambia pia kuwa tutaonana Majimbo ya Caucus" Alisema Paul ambaye nguvu zake kwa sasa amezielekeza katika majimbo ya Nevada, Colorado na Maine ambayo yapo katika ratiba ya kupiga kura wiki chache zijazo.

Ushindi huo wa Romney unamfanya kuwa mgombea Pekee kuongoza mara mbili katika kinyang'anyiro hicho kufuatia ushindi wake huko New Hampshire's tarehe 10 Januari. ushindi huo umeonesha uwezo wa Romney kushindana huku kura nyingi za maoni zikionesha  Romney anachagulika moja ya sababu zinazoaminika kuchangia ushindi huo wa Florida.

No comments:

Post a Comment