Wednesday, February 29, 2012

KINYANG'ANYIRO MGOMBEA URAIS KUPITIA REPUBLICAN-MICHIGAN WAPIGA KURA.

MICHIGAN, MAREKANI,
Mitt Romney mgombea anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa kukiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi ujao anasubiri hatima yake kutoka katika Jimbo la Michigan sehemu ambalo  alipozaliwa kujua kama atanyanyuka kidedea au atatupwa katika mbio hizo. Romney anapata upinzani mkali kutoka kwa Rick Santom ambaye anakabana nae koo kabla ya upigaji kura hapo jana Jumanne.

Baada ya kushinda katika jimbo la Arizona ambako alipata msaada mkubwa kutoka kwa Seneta wa jimbo hilo na mgombea wa urais kupitia tiketi ya Republican mwaka 2008 Bw. John McCain,  Romney anaiangalia Michigan kama moja ya mategemeo yake makubwa katika ushindi wake, huku maoni yakionesha mchuano mkali  kati yake na mpinzani wake huyo wa karibu.

 Endapo Santom atapata ushindi katika jimbo hilo litakuwa ni pigo kubwa mno kwa Romney na pengine itazua maswali mengi juu ya Uwezekano wa Romney kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo Romney anapewa nafasi zaidi dhidi ya Santom ambaye msimamo wake wa kidini na kutoaminika kama mgombea imara Dhidi ya Rais Obama vinampunguzia umaarufu.
Romney anaaminika kama Mchumi Imara kutokana na kuwa mfanyabishara maarufu akiwa na uzoefu wa miaka 25, na pia  kushika nafasi ya Gavana.
Akiongea katika kampeni zake Romney alinukuliwa akisema "Nitakwenda kushinda Michigan na nitashinda Nchi nzima"

kwa Upande wake Santom alisema amevutiwa na ushindani uliopo tangu mwanzo wa safari na jana wangeushangaza ulimwengu. Wagombea wengine Bw.Newt Gingrich na Ron Paul wameonekana kuachwa mbali katika mbio hizo kwa kutoa upinzani hafifu ambao umewaondoa katika mjadala kama wagombea wenye mvuto na upinzani. 

Mbio hizo ni za kumtafuta Mgombea Urais atakayepambana na rais aliyepo madarakani Bw.Barack Obama wa chama cha Democratic hapo Novemba Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment