Thursday, February 2, 2012

WATU 73 WAFARIKI KATIKA VURUGU ZA SOKA EGYPT


PORT SAID, EGYPT
       Watu 73 wameripotiwa kufa na wengine 1,000 kujeruhiwa katika vurugu kubwa za mchezo wa soka kati ya mashabiki wa Timu ya Al ahli iliyokuwa ikicheza dhidi ya timu ya  Al-Masry yenye maskani yake mjini humo. Vurugu hizo zimeibuka Mwisho wa mechi iliyoshuhudia timu ya Al-Masry Ikipata ushindi wa Magoli 3-1 dhidi ya wapinzani wao Al ahli.
Picha za televisheni zimeonesha mashabiki wa Timu ya Al-Masry Wakiingia Uwanjani na Kuwakimbiza Wachezaji wa Al ahli pamoja na mashabiki wao ambapo iliwalazimu kukimbilia kwenye chumba cha kubadilishia nguo hadi polisi walipokuja kuwaokoa na kuwatoa wakishirikiana na vikosi vya jeshi vilivyowasafirisha wachezji na majeruhi kwa helikopta. Shirikisho la mpira nchini humo limesogeza mbele baadhi ya mechi za ligi hiyo baada ya vurugu hizo huku Bunge likitarajiwa kukutan kesho kwa kikao cha dharura kujadili suala hilo.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Bw. Hosni Mubarak wametuhumiwa kuchochea vurugu hizo ingawa historia imeonesha uwepo wa matukio ya vurugu zinapokutana timu hizo, ingawa pia ukosefu wa Polisi umeonekana moja ya sababu za vurugu katika mechi za hivi karibuni nchini humo.

Mwanasheria mkuu wa Egypt ameagiza kufanyika uchunguzi mara moja juu ya tukio hilo huku naibu waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Hesham Sheiha akilitaja tukio hilo kuwa baya kabisa kupata kutokeaa katika Medani ya soka Nchini humo.

No comments:

Post a Comment