Sunday, July 29, 2012

KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAVUNJWA-Sababu ni ufisadi.

TANZANIA,
Kamati ya nishati na madini imevunjwa kwa tuhuma za ufisadi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kitangaza uamuzi huo spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda alisema vitendo kama hivyo havikubaliki hivyo anaivunja kamati hiyo ya nishati na madini na kupeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi ikiwemo uwezekano wa kutajwa kwa wabunge wanaohusika katika sakata hilo.

Hatua hiyo ilifuatia hoja ya Mbunge Vita Kawawa wa jimbo la Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na Bunge na Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe, hoja ambayo iliungwa mkono na spika huyo na kuvunja kamati hiyo.
Habari za fununu kutoka  Dodoma zimeeleza kuwa katika mlolongo huo wapo pia wabunge  wanaotoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, na wengine kutoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Wabunge waliochangia waliomba uchunguzi zaidi ufanyike na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

No comments:

Post a Comment