TANZANIA,
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimethibitisha kuwepo kwa mgomo wa walimu Tanzania kuanzia
hapo kesho licha ya serikali kutangaza kuwa mgomo huo ni batili.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa Baraza la CWT lilitoa notisi ya saa 48 ambazo zimemalizika leo mchana na hivyo kesho mgomo utakuwepo na walimu watatakiwa kubaki majumbani kwao bila kwenda kazini. Mukoba pia alisisitiza kuwa mgomo huo ni halali kwani wananachama waliopiga kura kuhalalisha mgomo walikuwa 153,000 ambapo kati ya 183,000 wakiwa sawa na asilimia 95.7 ya wanachama na hivyo kuhalalisha mgomo huo.
Rais huyo alimewataka walimu kutokuwa na hofu na ajira zao kwani mgomo huo umezingatia sheria.
Walimu wameingia katika mgomo huo wakiwa na madai ya ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa Sayansi asilimia 55, asilimia 50 pamoja na posho kwa walimu wa masomo ya sanaa na posho kwa walimu wanaoishi katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment