Jimbo la Zulu Natal |
Wachimba migodi wawili wameuawa na polisi nchini Afrika Kusini, wakati wa maandamano katika mgodi mmoja nchini humo , ikiwa ni tukio la hivi karibuni na vurugu mbaya.
Polisi wametuhumiwa kwa kuwafukuza wachimba migodi hao na kuwapiga risasi baada ya kujaribu kuvamia ghala la silaha karibu na eneo la Dannhauser mkoani Kwa Zulu Natal.Maafisa wanasema kuwa sasa wanachunguza mauaji ya watu wawili.
Migomo kadhaa imekumba sekta ya madini nchini humo na kuvuruga uzalishaji wa madini hali ambayo imeathiri uchumi wa nchi hiyo.
Wachimbaji ambao wamekuwa wakigoma wamekuwa wakikabiliana na poliisi katika vurugu mbaya sana.
Katika tukio mbaya zaidi kuripotiwa , zaidi ya watu 40 waliuawa mwezi Agosti, katika ghasia kati ya polisi na wachimba migodi wa mgodi wa Platinum waliokuwa wanagoma karibu na mgodi wa Rustenburg, ulio umbali wa kilomita 120 Magharibi mwa Johannesburg.
Katika tukio la hivi karibuni, takriban wachimba migodi 100 walikusanyika nje ya mgodi wa Ladybank karibu na Dannhauser.
Polisi walidaia kuwa baadhi ya wachimba migodi hao walijaribu kuvamia ghala la silaha kwa lengo la kuiba silaha hizo.
Walinzi wa serikali walituhumiwa kwa kuwafukuza wafanyakazi hao hadi katika mtaa mmoja wa mabanda na kuwafyatulia risasi pamoja na kuwajeruhi wengine
"Wanaume hao wawili walipelekwa hospitalii lakini walifariki muda mfupi baada ya kuwasili hospitalini’’ taarifa ya polisi ilielezea.
‘‘Polisi wanashika doria katika eneo hilo na wamenasa silaha kutoka kwa walinzi waliokuwa kazini kubaini nani waliofyatua risasi hizo’’
Afrika Kusini ni moja ya nchi inayozalisha madini mengi na ina kiwanda kikubwa cha mkaa.(Chanzo:BBC)
No comments:
Post a Comment