DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ameanza kutafuta suluhu kati ya viongozi wa dini za Kislamu na Kikristo ili kuweka misingi ya waumini wote kuheshimania na kudumisha amani nchini.
Prof. Lipumba amesema atafanya jitihada za kukutana na viongozi wa Kiislamu na Kikristo pamoja na wanasiasa akiwemo Rais Jakaya Kikwete ili kufikia lengo lake. Kiongozi huyo ameongeza kwamba, serikali ikitumia busara na kuwasiliana na Maimamu wa misikiti pamoja na viongozi wa Kikristo panaweza kupatikana tija. Lipumba amewaomba Waislamu wasishiriki kwenye maandamano baada ya Swala ya Ijumaa kwa kuwa hali hiyo ya mtafaruku ndiyo inayochochea ghasia na dhana kwamba Tanzania imetumbukia katika machafuko ya kidini.
Wiki iliyopita viongozi wa makundi mbalimbali ya waumini wa Kiislamu pamoja na polisi, walikuwa wakihimiza waumini kutojihusisha na maandamano hayo waliyoyaita haramu kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa amani. Waislamu wamekuwa wakiandamana wakitaka kuachiliwa huu Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye anaendelea kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi.(chanzo:Tehran)
No comments:
Post a Comment