PARIS -UFARANSA,
Nchi ya Ufaransa imekuwa nchi ya kwanza toka barani ulaya kulitambua rasmi baraza jipya la mapinduzi nchini Syria SNC ambalo lilitangaza viongozi wake wapya siku ya jumapili.
Akizungumza akiwa mjini Paris, rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa nchi yake inalitambua baraza hilo kama chombo halali kinachoongoza mapinduzi nchini Syria na sasa kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kuwasaidia waasi wa silaha.
Nchi nyingine za magharibi bado hazijatangaza kulitambua baraza hilo japo zimepongeza hatua ambayo imefikiwa na wajumbe wake kwa kujumuisha makundi yote yanayopigana nchini Syria.
Katika hatua nyingine mashambulizi zaidi yameripotiwa nchini Syria ambapo majengo ya shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi duniani UNHCR yameshambuliwa.
Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR na amesema kuwa licha ya hali ya usalama kutoridhisha nchini humo lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa msaada wa chakula na madawa.
No comments:
Post a Comment