Vurugu zilizozuka tangu juzi na kutulia kwa muda zilizuka tena hapo jana baada ya Mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki), Sheikh Musa Juma Issa kurudishwa rumande. Vijana waliokuwa wakipinga kurudishwa rumande kwa Mhadhiri huyo walichoma matairi barabarani na kuzua
tafrani.
Vurugu hizo zimetokea baada ya utulivu uliojitikeza baada ya Dk Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuitisha mkutano uliojumuisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi wa vurugu hizo.
Hata hivyo kitendo cha kurudishwa rumande kwa Sheikh Issa aliyeshindwa kutimiza masharti ya dhamana kulizua vurugu tena katika maeneo ya Mwanakeretwe na Amani .
Polisi walilazimika kutuliza vurugu hizo kwa kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya vijana hao
Hadi jana jioni, maeneo ya Chumbuni, Amani, Mwembaladu hali ilikuwa bado tete huku polisi wakifunga barabara kwa ajili ya kudhibiti vijana hao.

No comments:
Post a Comment