Katika mchezo huo azam fc iliwabidi wafanye mabadiliko ya mapema kwa kumpumzisha beki toka Kenya Jackson Atudo na nafasi yake kuchukuliwa na Lukson Kakolaki baada ya Atudo kuumia.
Katika dakika za mwanzo azam walichezea mpira katika eneo lao zaidi na kukaribisha mashambulizi ambayo yaliishia katika safu ya ulinzi ya azam fc iliyokuwa inaongoza na kipa Mwadini Ally.
Azam fc walifanya mashambulizi kadhaa katika lango la AS FAR katika kipindi hicho cha kwanza na kushindwa kuziona nyavu za wapinzani na kupelekea mpira kwenda mapumziko wakiwa suluhu.
Kipindi cha pili azam fc walizidisha masgambulizi katika lango la AS FAR, lakini uimara wa kipa wa waarabu hao walipelekea washamauliaji wa azam kushindwa kuingiza mpira kwenye nyavu za AS FAR.
Kipre Tchetche aliyepoteza nafasi mbili katika mchezo huo aligongesha mpira kwenye mwamba mara mbili katika dakika ya 53 na dakika za nyongeza.
Kocha wa azam fc Stewart Hall alifanya mabadiliko yaliyompeleka benchi Khamis Mcha aliyepoteza nafasi moja ya kuipatia goli azam fc na nafasi yake kuchukuliwa na Gaudence Mwaikimba, mabadiliko yaliyoshindwa kubadili matokeo na mchezo kwisha kwa sare ya bila kufungana.''
Azam na AS FAR wanataraji kurejeaana wiki mbili zijazo katika nchi ya Moroco ambapo azam wataitaji sare ya magoli ama washinde ili watinge katika hatua inayo fuata.
No comments:
Post a Comment