Friday, February 7, 2014

VIDEO:RAIS KIKWETE AKIFUNGUA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Thursday, February 6, 2014

SUMAYE KUGOMBEA URAIS? Ashindwa kukanusha, aipiga mkwara CCM.

sumaye 5afa9
MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimezidi kuibua mambo mapya, baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kudai atachukua uamuzi mgumu kama chama chake kitateua mgombea urais asiye na sifa.
Akizungumza Radio Tumaini, mjini Dar es Salaam jana asubuhi, Sumaye alisema kama CCM itafanya mambo ya ajabu kwa kuteua mgombea asiyekubalika wala kuwa na sifa za kiongozi mwadilifu, atafungua ukurasa mpya.
"Nitachukua uamuzi mgumu kama CCM watateua mgombea ambaye hana sifa ya kuwaongoza Watanzania, nitachukua uamuzi mgumu, haiwezekani tukaongozwa na watu wanaotoa fedha nyingi kila kukicha.
"CCM wakifanya mambo ya ajabu kwa kuchukua mtu ambaye ametoa fedha, nitatafuta njia nyingine," alisema.
Alisema hata siku moja hatakuwa na kinyongo kama atateuliwa mtu safi na mwenye moyo mweupe wa kusaidia Watanzania.
Alipoulizwa swali kama atagombea urais, alisema "Mimi sisemi kama nagombea, nakwambia muda ukifika nitasema tu, kwa wakati huu naomba tuendelee kutulia kwanza.
"Muda ukifika nitaamua nini cha kufanya, unajua unapotaka kuchukua uamuzi huu kuna mambo mazito ambayo unapaswa kuyatafakari kwa undani zaidi.
"Miongoni mwa mambo haya, ni kusaidia Watanzania kutoka walipo ili wapige hatua moja mbele zaidi, kuachana na tabia ya mtu mmoja kujitajirisha kupita kiasi," alisema Sumaye.
Alisema kama Watanzania wakimhitaji ili awasadie, atakuwa tayari kufanya hivyo.
"Muda ukiwadia na Watanzania wakisema wananihitaji, basi nami nitakuwa tayari kuwasaidia...jukumu hili linahitaji mtu mwenye busara sana," alisema Sumaye.
Alipoulizwa kuhusiana na hali ya CCM kwa sasa, alisema kuna tofauti kubwa katia ya CCM ya mwaka 1977 na ya sasa ambayo imekuwa ikikumbwa na matukio mengi.
Akitoa mfano, alisema: "Hivi sasa ukitaka kugombea lazima uwe na fedha, haya ni mambo machafu ambayo CCM yetu ya miaka ya 77 haikuwapo kabisa.
"Nalisema hili kutoka moyoni mwangu, nimekuwa mbunge na mjumbe wa NEC kwa miaka 20, sijawahi kutoa rushwa wala kupokea.
"Ukiona watu hao wanatoa rushwa, ujue moja, hawana uwezo wa kuongoza wananchi wao na ndani ya mioyo yao hawana dhamira safi zaidi ya kutanguliza maslahi yao.
"Nikikuhonga leo ujue sina nia njema, sitakuhudumia pindi nitakapoingia madarakani, nitaanza kwanza kutafuta namna ya kurudisha fedha zangu... hii ni vita ambayo CCM tunapaswa kuipinga kwa nguvu zote," alisema Sumaye.
MUUNDO WA SERIKALI
Akizungumzia muundo wa Serikali, alisema yeye ni muumini wa muundo wa serikali mbili siku zote na atendelea kusimamia ukweli huo.
"Haiwezekani ndani ya taifa hili tukawa na serikali tatu, hivi Rais wa Jamhuri ambaye anamiliki mali nyingi, akisema anamnyima Rais wa Tanganyika misaada nini kitatokea... huu ndio mwanzo wa kuondoa utulivu wetu, tuwe makini, tutaparanganyika," alisema Sumaye.
RUSHWA
Kuhusu rushwa, alisema wakati wa utawala wa awamu ya tatu, chini ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, walipambana vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kuondoa kipengele cha takrima.
"Tumepambana vya kutosha dhidi ya rushwa, hata takrima tulihakikisha inaondolewa wakati ule baada ya kubaini uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulijumuisha madiwani, ndiko hali hiyo ilikuwa imejikita.
"Nakumbuka enzi za utawala wangu, niliagiza idara zote za serikali mikoani na wilayani kukutana kwa saa moja kujadiliana masuala ya rushwa na ugonjwa wa Ukimwi," alisema Sumaye.
MAWAZIRI MIZIGO
Akizungumzia utendaji kazi wa awamu yake, Sumaye alisema ndani ya Baraza la Mawaziri hakukuwa na mawaziri mizigo.
"Sikuwa na mawaziri mizigo kwenye utawala wangu, utaona hata umma kwa sehemu kubwa unakiri tulifanya kazi nzuri.
"Nakwambia ukiwa na mizigo unapaswa kuitua haraka sana kabla ya watu hawajakuona," alisema Sumaye.
WAPINZANI
Kuhusu vyama upinzani, Sumaye alisema vimekuwa na mchango mkubwa wa kuimarisha serikali katika utekelezaji wa mambo muhimu.
"Siku zote nimekuwa muumini mkuu wa upinzani, wamekuwa kiungo muhimu, natamani kuona wanaingia kwa wingi kwenye Bunge letu, michango yao mizuri...nawaomba waendelee hivi hivi wasirudi nyuma," alisema Sumaye.
MBOWE
Kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwamba Katiba itapatikana kwa ngumi, Sumaye alisema kauli hiyo si nzuri, kwa sababu amani ikitoweka, si CCM wala CHADEMA watakaopona.
"Nimemsikia akiruka na helikopta zake huko mikoani na kusema atatumia nguvu, hivi jamani leo amani ikitoweka, CCM na CHADEMA watapona?" Alihoji Sumaye. Chanzo: mwananchi

KWA NINI MANDELA ALIMUACHA WINNIE KATIKA MGAWANYO WA URITHI?


                   Graca akiwa na Winnie Mandela katika Msiba wa Mandela
JOH'BURG-AFRIKA KUSINI,
Wosia wa Mandela aliouandika mwaka 2004, umetangazwa hivi karibuni, ukishuhudia mke wa pili wa Mandela mama Graca Machel akipata nusu ya mali zote alizokuwa akimiliki mpigania uhuru huyo wa Afrika Kusini.Mali nyingine pia zimeende kwa watoto wa Mandela na wale wa Graca aliozaa na Samora machel.Mali nyingine zimeenda kwenye

Hata hivyo mshangao mkubwa umeonekana katika suala la mgao wa mali kwenda kwa mtalaka wa Mandela, Winnie Mandela  ambaye hajapewa kitu katika mgao huo! Winnie ambaye alikuwa karibu na Mandela katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ubaguzi Afrika kusini, huku akijizolea sifa ya ushujaa kwa kuwa mwanamke aliyemsubiri mume wake kwa kipindi cha miaka 27 akiwa jela, jina lake halijaonekana katika wosia huo.

Katika wosia huo ambao hadi wajukuu wa Mandela pamoja na watoto wa Graca aliozaa na Samora Machel wamepewa urithi wao inashangaza sana kuona mwanamke huyo ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Mandela akiachwa bila kitu.

Maswali mengi yanazunguka katika vichwa vya watu; ni kwa nini Mandela aliweza kuwasamehe wabaya wake waliomtesa enzi za kupigania uhuru na akashindwa kumsamehe mke wake wa ndoa aliyemvumilia kipindi chote hicho? ni kosa gani kubwa la kiasi hicho Winnie alimfanyia Mandela?

Wednesday, February 5, 2014

UTATA WAIBUKA KESI YA MTANZANIA DHIDI YA MKE WA JACOB ZUMA.

Rais Zuma na Mkewe Nompumelelo Ntuli Zuma

JOH'BURG-AFRIKA KUSINI, Kesi ya Mtanzania Stephen Ongolo anayeshikiliwa na polisi Afrika Kusini akituhumiwa kutishia kutoa siri za mke wa pili wa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli Zuma (MaNtuli), imeibua mabishano ya kisheria ya kuhusu mahali anapotakiwa kushtakiwa.
Gazeti la The Star la Afrika Kusini liliripoti kuwa baada ya Ongolo kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Camperdown jijini Durban, Jumatatu wiki hii, ilibainika kuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ndoda January hakueleza ni wilaya gani ya kimahakama ambayo Ongolo alitenda kosa hilo. January alisema kuwa walishindwa kujua eneo alilofanya makosa Ongolo, kwani alikuwa akitumia ujumbe mfupi wa simu alioutuma kwa vyombo vya habari vya nchi hiyo.
"Tunashindwa kuelewa eneo gani ambalo mshtakiwa amefanya kosa kwa sababu mlalamikaji anaweza kuwa sehemu yeyote kati ya Camperdown na Nkandla ambako alipeleka ujumbe huo," alisema January.

Kukamatwa kwa Ongolo
Ongolo alikamatwa na polisi jijini Durban mwezi uliopita kwa madai ya kumtishia mke wa pili wa Rais Zuma kuwa angetoa siri zake. Siri hizo zinahusiana na kifo cha mlinzi wa Rais Zuma, Phinda Thomo, ambaye alidaiwa kujiua bafuni kwake mwaka 2009.
Ongolo alikaririwa na Gazeti la Sunday Independent la Afrika Kusini akieleza kuwa Thomo hakujiua bali kifo chake kilipangwa baada ya siri kati yake na MaNtuli kubainika.
Gazeti la The Star la nchini humo, jana liliripoti kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Thys Talijaard wa Camperdown alisema ili Ongolo apate dhamana hapo Camperdown, alitakiwa awe ameshtakiwa kwa makosa aliyofanya kwenye mahakama ya wilaya ambayo kosa limetendeka.
Ongolo alitakiwa kuomba dhamana Jumatatu lakini mwanasheria anayemtetea, Lekoa Le-koko hakuwapo mahakamani, na hivyo mashtaka kupangwa kusikilizwa tena jana.
Wakati mshtakiwa huyo akiwa mahakamani hapo ulizuka mjadala mzito kati ya January na Mdu Thuketana ambaye alishika nafasi ya Le-koko, wakijadiliana ni wapi mshtakiwa anaweza kushikiliwa wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa.
Thuketana aliomba Ongolo awe chini ya ulinzi wa polisi kutokana na afya yake kwani anasumbuliwa na maradhi ya pumu na pia walikuwa wakihofia usalama wake.
Wiki iliyopita, Ongolo alishindwa kwenda mahakamani baada ya kuugua pumu na kupelekwa hospitali.
Hata hivyo, January alisema mshtakiwa anaweza kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa siku saba tu, na baada ya hapo atapelekwa kwenye mahabusu za kawaida, jambo ambalo liliafikiwa na Hakimu Talijaard.
Kuhusu uraia wa Ongolo, Msemaji wa Ofisi ya Uhamiaji nchini Tanzania, Kamishna Abbas Irovya alisema suala la uraia wake linatakiwa lianzie Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambako yuko, badala ya kuanzia hapa nchini.
"Kama ubalozi haumtambui, hata sisi inakuwa shida kwetu kuthibitisha." alisema.
Chanzo:Mwananchi

MTANDAO WA KIJAMII WA FACEBOOK WATIMIZA MIAKA 10

MarkZuckerberg_588a9.jpg
                         Mark Zuckerberg alianzisha Facebook kwenye Harvard chumba cha bweni

Facebook ni mtandao wa Kijamii, ambao unatokana na jina la colloquial name for the book ulianzishwa nchini marekani kwa ajili ya wanafunzi ili uweze kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kuwasiliana na kutambuana kila mmoja.
It was founded in February 2004 by Mark Zuckerberg with his college roommates and fellow Harvard University students Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz and Chris Hughes.
Mtandao huu ulianzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard, lakini baadaye ulipanuka hadi vyuo vingine vya maeneo ya Boston, the Ivy League, naStanfordUniversity. Hatua kwa hatua ulizi kuungwa mkono na wanafunzi kwa kuongeza usaidizi kabla ya kufunguliwa katika vyuo vikuu vingine, na hatimae kufukia kwa kila mmoja mwenye kufikia umri wa miaka 13 na zaidi. Facebook kwa sasa inaruhusu mtumiaji yeyote ambao watabainisha angalau kutimiza miaka 13 ili wajisajili katika facebook kama watumiaji.

Tuesday, February 4, 2014

NATO yamuonya Karzai 'kutocheza na moto'

 

Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO Anders Fogh Rasmussen amemuonya Rais wa Afhaganistan Hamid Karzai kuwa 'anacheza' na moto.

Hii ni baada ya kiongozi huyo kukataa kutia saini mkataba utakaowaruhusu wanajeshi wa NATO kuendelea kuhudumu hata baada ya kukamilika kwa muda waliokubaliana awali wa mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza na BBC Anders Fogh Rasmussen alisema amepigwa na butwaa na matamshi ya Rais Karzai kuhusiana na majeshi ya Jumuiya Kujihami ya NATO .

''mimi na rais Karzai ni marafiki mno lakini sikubaliani naye kwani hatua yake itarudisha nyuma juhudi za jamii ya kimataifa ya kuleta amani Afghanistan.

Unajua kuwa Nato imewekeza kwa hali mali na damu ya majeshi kuilinda Afghanistan nafikiri jamii ya kimataifa inahitaji shukrani sio habari kama hizo.

                                                                Wanajeshi wa NATO

'' Iwapo Rais Karzai ana mipango ya kukataa kutia saini makubaliano hayo basi ni sharti ajiandae kugharamia mishahara ya wanajeshi wa Afghanistan pamoja na polisi kwani NATO imeitengeza jeshi la Afghanistan hadi kufikia idadi ya majeshi laki tatu u nusu .

Serikali ya Afghanistan haina uwezo huo .

Rusmussen aliambia BBC kuwa Majeshi ya Mungano yamewekeza kwa kiwango kikubwa kwa amani ya taifa hilo na hata iwapo Karzai atakataa kuidhinisha mkataba huo ana imani kuwa Rais atakayechaguliwa Mwezi Machi hatakuwa na budi ila kuweka saini.
Gazeti moja lilimnukuu Rais Karzai akisema kuwa jimbo la Helmand lilikuwa na amani Hadi majeshi ya Uingereza chini ya NATO yalipoingia huko .(chanzo:bbc swahili)

WOSIA WA MANDELA WATANGAZWA-

Johannesburg. Wosia wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela umesomwa huku mgawanyo wa mali zake ukielekezwa katika maeneo tofauti.
Katika wosia huo uliosomwa rasmi jana, Mandela aliacha mali zenye thamani ya Dola za Marekani 4.1 milioni, sawa na Sh5.6 bilioni ambazo zimepangwa kugawiwa kwa taasisi mbalimbali, familia na wafanyakazi wake.
Katika wosia huo ulioandikwa na Mandela mwenyewe mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2008, mkewe, Graca Machel anapata karibu nusu ya mali zake zote alizoziacha.
Mali hizo zinajumuisha nyumba kubwa alizokuwa akimiliki moja ikiwa Johanesburg, nyingine Qunu na ya tatu Mthatha. Mali nyingine ni sehemu ya mrabaha aliyokusanya baada ya kuuza machapisho mbalimbali ikiwamo kitabu chake maarufu cha “Long Walk to Freedom” ambacho kinatajwa kuuzwa kwa wingi duniani.
Pia sehemu za mali hizo zimetokana na kazi mbalimbali alizozifanya wakati akiwa rais na baada ya kuachia madaraka na kujihusisha na wakfu wake wa Mandela Foundation. Wakfu huo ndiyo uliofanikisha kuratibu shughuli mbalimbali za kijamii ambazo alizitekeleza baada ya kustaafu.
Kutangazwa kwa mali hizo kumemaliza minong’ono ya muda mrefu iliyokuwa ikihusisha sehemu kubwa ya familia yake ambayo imewahi kuingia kwenye malumbano juu ya nani anayepaswa kumiliki mali hizo.
Akisoma wosia ulioachwa na Mandela mbele ya waandishi wa habari, Naibu Jaji Mkuu Dikgang Moseneke alisema wanafamilia ya Mandela wamekubaliana na yote yaliyoandikwa na hakuna pingamizi lolote lililotijokeza.
Hata hivyo, kuna nafasi ya kuweka pingamizi juu ya wosia huo katika kipindi cha siku 90 kuanzia sasa vinginevyo, baada ya hapo utaanza kutekelezwa mara moja.
Wosia huo uliokuwa na kurasa 40 umeorodhesha watu na taasisi zinazostahili kuwa sehemu ya mgawanyo huo wa mali na kutaja kiwango stahili kinachopaswa kutolewa.
Chama cha ANC ambacho Mandela na marafiki zake walikiasisi kwa ajili ya kukabiliana na siasa za kibaguzi wakati wa utawala wa makaburu ni miongoni mwa taasisi ambazo zitapitiwa na mgawo huo.
Kamati Kuu ya ANC inatazamia kutumia fedha hizo kwa ajili ya kusambaza sera na misingi ya chama inayohusu maridhiano.
Wengine waliotajwa kwenye urithi huo ni pamoja na aliyekuwa msaidizi wake katika siku zake za mwisho, Zelda la Grange, Chuo Kikuu cha Wits, Shule ya Sekondari ya Qunu na Shule ya Sekondari ya Orlando iliyoko Soweto.