NATO yamuonya Karzai 'kutocheza na moto'
Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO Anders Fogh Rasmussen amemuonya Rais wa Afhaganistan Hamid Karzai kuwa 'anacheza' na moto.
Hii ni baada ya kiongozi huyo kukataa kutia saini mkataba utakaowaruhusu wanajeshi wa NATO kuendelea kuhudumu hata baada ya kukamilika kwa muda waliokubaliana awali wa mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza na BBC Anders Fogh Rasmussen alisema amepigwa na butwaa na matamshi ya Rais Karzai kuhusiana na majeshi ya Jumuiya Kujihami ya NATO .
''mimi na rais Karzai ni marafiki mno lakini sikubaliani naye kwani hatua yake itarudisha nyuma juhudi za jamii ya kimataifa ya kuleta amani Afghanistan.
Unajua kuwa Nato imewekeza kwa hali mali na damu ya majeshi kuilinda Afghanistan nafikiri jamii ya kimataifa inahitaji shukrani sio habari kama hizo.
'' Iwapo Rais Karzai ana mipango ya kukataa kutia saini makubaliano hayo basi ni sharti ajiandae kugharamia mishahara ya wanajeshi wa Afghanistan pamoja na polisi kwani NATO imeitengeza jeshi la Afghanistan hadi kufikia idadi ya majeshi laki tatu u nusu .
Serikali ya Afghanistan haina uwezo huo .
Rusmussen aliambia BBC kuwa Majeshi ya Mungano yamewekeza kwa kiwango kikubwa kwa amani ya taifa hilo na hata iwapo Karzai atakataa kuidhinisha mkataba huo ana imani kuwa Rais atakayechaguliwa Mwezi Machi hatakuwa na budi ila kuweka saini.
Gazeti moja lilimnukuu Rais Karzai akisema kuwa jimbo la Helmand lilikuwa na amani Hadi majeshi ya Uingereza chini ya NATO yalipoingia huko .(chanzo:bbc swahili)
No comments:
Post a Comment