Graca akiwa na Winnie Mandela katika Msiba wa Mandela
JOH'BURG-AFRIKA KUSINI,
Wosia wa Mandela aliouandika mwaka 2004, umetangazwa hivi karibuni, ukishuhudia mke wa pili wa Mandela mama Graca Machel akipata nusu ya mali zote alizokuwa akimiliki mpigania uhuru huyo wa Afrika Kusini.Mali nyingine pia zimeende kwa watoto wa Mandela na wale wa Graca aliozaa na Samora machel.Mali nyingine zimeenda kwenye
Hata hivyo mshangao mkubwa umeonekana katika suala la mgao wa mali kwenda kwa mtalaka wa Mandela, Winnie Mandela ambaye hajapewa kitu katika mgao huo! Winnie ambaye alikuwa karibu na Mandela katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ubaguzi Afrika kusini, huku akijizolea sifa ya ushujaa kwa kuwa mwanamke aliyemsubiri mume wake kwa kipindi cha miaka 27 akiwa jela, jina lake halijaonekana katika wosia huo.
Katika wosia huo ambao hadi wajukuu wa Mandela pamoja na watoto wa Graca aliozaa na Samora Machel wamepewa urithi wao inashangaza sana kuona mwanamke huyo ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Mandela akiachwa bila kitu.
Maswali mengi yanazunguka katika vichwa vya watu; ni kwa nini Mandela aliweza kuwasamehe wabaya wake waliomtesa enzi za kupigania uhuru na akashindwa kumsamehe mke wake wa ndoa aliyemvumilia kipindi chote hicho? ni kosa gani kubwa la kiasi hicho Winnie alimfanyia Mandela?
No comments:
Post a Comment