DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Aliyewahikuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili baada ya upande wa mashitaka kuonekana hauna ushahidi wa kujitosheleza.
Prof.mahalu ambaye alikuwa akishitakiwa na serikali kwa kuisababishia hasara ya Euro 2,065,827.60, kwa manunuzi ya majengo ya Balozi nchini Italia kinyume cha sheria.
.
Akisoma hukumu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Ilvine Mugeta, amesema Profesa Mahalu na aliyekuwa Mkuu wa Fedha na Utawala katika ubalozi huo, Bi.Grace Martin, hawajapatikana na hatia kwa kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haujajitosheleza na kulingana na hivyo kuwa si wa kweli.
Kwa kigezo hicho hakimu huyo amewaachia huru washitakiwa hao kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
No comments:
Post a Comment