TABORA-TANZANIA,
Mahakama kuu Kanda ya Tabora imetengua rasmi matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi wa kiti cha ubunge mgombea na aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) Dk Peter Kafumu, katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Hukumu hiyo imefuatia kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea katika uchaguzi huo kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na Maendeleo Profesa Abdalla Safari aliyemshitaki mgombea, huyo, mwanasheria mkuu wa Serukali, na msimaizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika kesi hiyo hoja mbalimbali zilitolewa kupinga matokeo hayo ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka kwa Waziri wa Ujenzi John Magufuli kufanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga na kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi na kuwatisha wananchi kuwa wasipoichagua CCM watashughulikiwa.
Katika hoja nyingine mgombea huyo kupitia tiketi ya CHADEMA akiwakilishwa na wakili wake walimshitaki Rais mstaafu Benjamini Mkapa aliyetoa ahadi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla ya Uchaguzi, pamoja na ile ya baraza la Waislamu (Bakwata) wilaya ya Igunga kuwakataza waumini wake wasikipigie kura chama cha CHADEMA.
No comments:
Post a Comment