Friday, August 24, 2012
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA NORWAY AFUNGWA MIAKA 21.
OSLO-NORWAY,
Mahakama nchini Norway imemkuta na hatia na kumhukumu kifungo cha miaka 21 jela, mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway Bw.Anders Behring Breivik. Matuhumiwa huyo alidaiwa kuhusika na mauaji ya watu 77 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 240 wakati alipotega bomu katikati ya mji wa Oslo na baadae kuwapiga kwa risasi vijana waliokuwa katika kambi moja huko Camp Island.
Mtuhumiwa huyo alikiri kufanya makosa hayo na kukataa kuitwa mkosaji akitetea uamuzi wake kuwa ni sahihi kwa kuwa alikuwa akizuia kuenea Uislam Norway.Kesi hiyo ambayo imedumu kwa miezi kadhaa ilikuwa na mvutano ambapo licha ya kuonekana na hatia mawakili na serikali walikuwa na mvutano ikiwa mtuhumiwa huyo yupo timamu au ana matatizo ya akili hali iliyokuwa ikileta utata juu ya hukumu anayostahili, ingawa hatimaye serikali imajiridhisha kuwa mtuhumiwa huyo anastahili hukumu.
Hukumu hiyo imewekwa wazi ambapo itaweza kuongezwa kwa miaka zaidi ya 21 ikiwa mtuhumiwa huyo ataonekana bado ni hatari kwa jamii yake hata baada ya kumaliza kifungo chake.
Familia na ndugu wa Marehemu na waathirika wa tukio hilo wameridhishwa na hukumu hiyo,"Amepata anachostahili," alisema Alexandra Peltre, 18,ambaye alipigwa risasi na kujeruhiwa na mtuhumiwa huyo.Bi. Per Balch Soerensen, ambaye binti yake aliuawa katika shambulio hilo alisema anashukuru hukumu hiyo imefika mwisho kwa sababu watakuwa na amani na utulivu tena.
Mtuhumiwa huyo akivalia sare kama za polisi alilipua bomu pamoja na kuwapiga risasi vijana waliokuwa katika kambi huko Norway, na kusababisha vifao vya watu 77 hapo mwezi Julai Mwaka jana.
Labels:
habari mpya,
kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment