Monday, March 12, 2012

Mgomo wa madaktari wafikia kikomo- Juhudi za Kikwete zaokoa Jahazi.

(Picha kwa hisani ya IPP Media)

CHAMA cha Madaktari Tanzania (Mat) kimetangaza kusitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia juzi siku ya jumamosi mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kumheshimu Rais Jakaya Kikwete, huku kikiwatangaza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya kuwa maadui namba moja wa sekta ya afya nchini.

Uamuzi huo wa kurejea kazini umekuja siku  moja baada ya viongozi wa MAT na Jumuiya ya madaktari Tanzania kukutana na Rais Kikwete Ikulu kujadili mgogoro huo, ikiwa ni siku ya nne tangu madaktari hao walipoanza mgomo kwa mara ya pili, wakishinikiza Serikali kutekeleza madai yao, likiwemo la Dk Mponda na Dk Nkya kujiuzulu.

Hata hivyo haikufahamika kwa undani juu ya kilichokubaliwa ingawa Rais wa MAT ndugu Namala Mkopi alisema wamemweleza rais madai yao kwa undani na ameyasikiliza na kuyachukulia kwa uzito madai yao.
Baada ya tangazao hilo  huduma zimedaiwa kuanza kurudi katika hali ya kawaida katika baadhi ya hospitali hususani zile za Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment