Friday, March 30, 2012

ECOWAS WAHAIRISHA MKUTANO WA MALI.

Wawakilishi wa Umoja wa Kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wamehairisha mkutano wao na viongozi wa seriali ya uasi ya Mali uliokuwa ufanyike nchini humo na sasa watakutana Mjini Abidjan Ivory Coast.Kwa Mujibu wa Taarifa za Ikulu kutoka nchini Ivory Coast hali ya usalama nchini Mali yakiwemo maandamano ya Kuunga mkono mapinduzi ni moja ya sababu za Kuhamishwa Mkutano huo.
Imeripotiwa kuwepo kwa maandamano makubwa katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako na  uwanja wa ndege nchini Mali katika eneo la kupaa na kutua hali inayofanya usafiri kuwa mgumu kwa njia ya anga nchini humo.
Siku ya Jumatano maelfu ya wananchi wa Mali waliandamana kupinga kuingiliwa na nchi za kigeni huku wakiyaunga mkono maandamano hayo.
Waasi nchini humo waliipindua serikali ya rais Toure kwa kile walichokiita kushindwa kushughulikia suala la waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi hiyo ambapo tayari viongozi hao wa mapinduzi wametangaza kuwepo kwa katiba mpya huku sehemu kubwa ya vifungu katika katiba ya zamani vikiwemo ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza na kutembea,pia  wametangaza kuwepo kwa uchaguzi ingawa waliohusika katika mapinduzi awataruhusiwa kushiriki uchaguzi huo.
Wakati huo huo nchi jirani na Mali zikiwemo Ivory Coast na ghana  zimetishia kufunga mipaka yao inayopakana na nchi hiyo kuanzia saa72 zijazo ikiwa majeshi ya waasi hayatakabidhi madaraka kwa wananchi.Pia nchi zote za ECOWAS zimesema zitaizuia mali kutumia bandari zao katika usafiridhaji. Kikwazo kingine ni kufungwa kwa akaunti ya serikali ya nchi hiyo katika benki ya Ukanda wa magharibi ya ECOWAS pia benki hiyo imezuiwa kutoa pesa kwa benki binafsi nchini Mali.

Monday, March 12, 2012

Mgomo wa madaktari wafikia kikomo- Juhudi za Kikwete zaokoa Jahazi.

(Picha kwa hisani ya IPP Media)

CHAMA cha Madaktari Tanzania (Mat) kimetangaza kusitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia juzi siku ya jumamosi mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kumheshimu Rais Jakaya Kikwete, huku kikiwatangaza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya kuwa maadui namba moja wa sekta ya afya nchini.

Uamuzi huo wa kurejea kazini umekuja siku  moja baada ya viongozi wa MAT na Jumuiya ya madaktari Tanzania kukutana na Rais Kikwete Ikulu kujadili mgogoro huo, ikiwa ni siku ya nne tangu madaktari hao walipoanza mgomo kwa mara ya pili, wakishinikiza Serikali kutekeleza madai yao, likiwemo la Dk Mponda na Dk Nkya kujiuzulu.

Hata hivyo haikufahamika kwa undani juu ya kilichokubaliwa ingawa Rais wa MAT ndugu Namala Mkopi alisema wamemweleza rais madai yao kwa undani na ameyasikiliza na kuyachukulia kwa uzito madai yao.
Baada ya tangazao hilo  huduma zimedaiwa kuanza kurudi katika hali ya kawaida katika baadhi ya hospitali hususani zile za Dar Es Salaam.

Mgomo wa madaktari wafikia kikomo- Juhudi za Kikwete zaokoa Jahazi.

(Picha kwa hisani ya IPP Media)
CHAMA cha Madaktari Tanzania (Mat) kimetangaza kusitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia juzi siku ya jumamosi mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kumheshimu Rais Jakaya Kikwete, huku kikiwatangaza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya kuwa maadui namba moja wa sekta ya afya nchini.

Uamuzi huo wa kurejea kazini umekuja siku  moja baada ya viongozi wa MAT na Jumuiya ya madaktari Tanzania kukutana na Rais Kikwete Ikulu kujadili mgogoro huo, ikiwa ni siku ya nne tangu madaktari hao walipoanza mgomo kwa mara ya pili, wakishinikiza Serikali kutekeleza madai yao, likiwemo la Dk Mponda na Dk Nkya kujiuzulu.

Hata hivyo haikufahamika kwa undani juu ya kilichokubaliwa ingawa Rais wa MAT ndugu Namala Mkopi alisema wamemweleza rais madai yao kwa undani na ameyasikiliza na kuyachukulia kwa uzito madai yao.
Baada ya tangazao hilo  huduma zimedaiwa kuanza kurudi katika hali ya kawaida katika baadhi ya hospitali hususani zile za Dar Es Salaam.

Friday, March 9, 2012

WAKE WA OSAMA WASHITAKIWA.

Nyumba aliyokuwa akiishi Osama bin Laden ambayo baadae ilibomolewa.

Islamabad, Pakistan.
Wake watatu wa Osama Bin Laden wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Kuingia na kuishi nchini Pakistani kinyume cha sheria . Wanawake hao ambao wawili kati yao ni raia wa Yemen na mmoja wa Saudi Arabia ni miongoni mwa watu 16 waliokamatwa baada ya  kikosi maalum cha Marekani kuvamia nyumba aliyokuwa akiishi Osama Bin Laden na familia yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan mwezi mei mwaka jana wanashikiliwa na serikali ya Pakistan.
Kwa Mujibu wa waziri wa Mambo ya ndani ya Pakistan Bw.Rehman Malik wanawake hao tayari wamefunguliwa mashitaka katika mahakama ambayo hakutaka kuitaja kwa sababu za kiusalama  na kuongeza kuwa wanahaki ya kumtafuta Wakili atakayewatetea katika kesi hiyo.

"Wamefikishwa mahakamani na baada ya hapo sheria ndio itakayoamua, hata hivyo kesi hiyo itawahusu wao pekee na watoto hawatoshitakiwa ....... Pia wanaweza kuwa na wakili na wana uhuru kamili wa kujitetea wenyewe mbele ya mahakama"

Waziri huyo hakutaja ni adhabu gani ambayo itawakabili wanawake hao endapo watapatikana na hatia ingawa kwa Mujibu wa Sheria za Pakistan wanaweza kukabiliwa na kifungo cha Hadi Miaka kumi (10) na faini ya dola 110 kila mmoja.

         Hatima ya Watoto?
Kuhusu hatima ya watoto Bw.Malik amesema  wamewekwa katika nyumba salama  yenye vyumba vitano (5) vya kulala na wanapata mahitaji na haki zote kama nyumbani na wataweza kurudishwa katika nchi zao ikiwa mama zao watakubali.

MGOMO WA MADAKTARI MOTO! - Pinda ahairisha Ziara Mwanza.

  Mmoja wa wagonjwa Bi. Fatuma Rashid akiondoka eneo la hospitali ya 
Temeke baada ya kukosa Huduma (Picha kwa hisani ya IPP Media)






Dar es Salaam, Mgomo wa madaktari ulioanza kwa kasi ndogo hapo juzi umeanza kushika kasi baada ya hapo jana idadi ya Hospitali zilizoripotiwa kuwa na mgomo huo kuongezeka kutoka zile za awali za Bugando na Amana mpaka Muhimbili, Temeke na Hospitali nyingine za Rufaa Mikoani huku Hospitali ya Muhimbili  hapo jana ikitangaza rasmi kuifunga Kliniki yake ya Wagonjwa wa nje kutokana na Uchache wa madaktari , hali hiyo imedaiwa kumlazimu Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda Kuhairisha ziara yake ya siku kumi mkoani Mwanza ili kushughulikia tatizo la hilo mara moja. Kwa Mujibu wa Vyanzo vya ndani Waziri mkuu amehairisha ziara yake hiyo hadi hapo itakapotangazwa tena.

Idadi ndogo ya wagonjwa Imeripotiwa katika Hospitali za Serikali kutokana na mgomo huo ambapo katika baadhi ya Hospitali ikiwemo Muhimbili wagonjwa waliolazwa wameondolewa na ndugu na jamaa zao kwenda kwenye hospitali binafsi na Wengine nyumbani, mmoja wa ndugu aliyetambulika kwa jina  Marwa Chacha  alisema ameamua kumuhamisha mama yake mzazi kutoka Muhimbili kwenda Hospitali ya Regency kutokana na kuzorota kwa huduma katika hospitali hiyo, nae Filbert Tarimo aliyekuja Muhimbili kutoka Morogoro kwa matibabu ya Moyo aliambiwa arudi nyumbani mpaka atakapopewa taarifa tena.
  Huko Mwanza katika Hospitali ya Rufaa ya bugando madaktari hapo jana waliendelea na Mgomo wao kwa siku ya pili na kusababisha usumbufu mkubwa kwa Wagonjwa, huku mmoja wa Madaktari wa Hospitali hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake akisema madaktari hao pia wamegomea Kikao kilichoitishwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo hapo jana mchana.
. “Leo tuliitwa kwenye kikao na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, lakini tulikubaliana tusifike kwenye kikao hicho hivyo hatutakwenda,” alieleza mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka kuandikwa gazetini kwa kile alichoeleza kuwa sasa sio wakati wa kuandikana majina kwenye vyombo vya habari.  Huduma katika hospitali hiyo jana zilianza kuzorota kwani licha ya baadhi ya madaktari wa kidini ambao sio waajiriwa wa Wizara ya afya kutogoma hali ilikuwa mbaya kutokana na  kuzidiwa kwa madaktari hao.

Iringa - katika hospitali ya rufaa ya Iringa kumeripotiwa pia  kuwepo kwa mgomo ambapo licha ya madaktari  kuwepo katika mazingira ya hospitali hiyo hawakutoa huduma yoyote kwa wagonjwa waliofika kupata huduma hiyo, Wakati Mkoani Tanga katika Hospitali ya Bombo hali kama hiyo pia ikiripotiwa.

Chama cha wafanyakazi TUGHE kupitia kwa katibu wake kimesema mgomo huo ni matokeo ya kutoaminiana kati ya serikali na Madaktari hao huku akiitaka serikali kushughulikia suala hilo kama chombo cha umma, akisisitiza Umuhimu wa pande zote mbili kukaa na kufikia makubaliano tena ili kunusuru maisha ya watanzania.
Wananchi wengi waliotoa maoni wamepeleka lawama zao kwa Serikali na madaktari hao huku wengine wakitaka kuwajibishwa au kuwajibika kwa mawaziri hao.

Hadi hapo jana serikali ilikuwa kimya na hakuna tamko rasmi tangu lile la Waziri Mkuu kabla ya kuanza kwa mgomo huo na wananchi wengi wanasubiri kwa hamu kujua hatua gani serikali itaichukua kunusura hali zao.

Thursday, March 8, 2012

KULIKONI YATAWALA AFYA YA LOWASSA!

DAR ES SALAAM, Kumekuwa na habari za utata kuhusu hali ya afya ya Waziri mkuu aliejiuzulu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, huku baadhi ya habari zikitaarifu kuwa mbunge huyo amelazwa katika hospitali huko ujerumani. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi hapo jana tarehe 7 Machi, limefanikiwa kuzungumza na Mbunge huyo ambaye alikiri kuwepo hospitalini ingawa alikataa kuelezea kwa undani kuhusu hali yake ya afya. Alipoulizwa kuhusu suala hilo katibu wa bunge Dk Thomas Kashillilah alisema ofisi yake haina taarifa juu ya suala hilo. Hali hiyo bado inazua maswali mengi lakini pengine tuendelee kuvuta subira juu ya taarifa rasmi ya kinachoendelea.