Monday, January 30, 2012

MAPIGANO SYRIA- MAJESHI YA SERIKALI YAUTWAA MJI WA DAMASCUS

DAMASCUS,SYRIA- Majeshi ya serikali yamefanikiwa kutwaa baadhi ya vitongoji vitongoji vya mji wa Damascus kutoka kwa waasi wa kundi la Free Syrian Forces hapo jana baada ya mapigano yaliyodumu kwa muda wa siku mbili na kushuhudia mauaji ya Jumla ya watu 66 wakiwemo raia 26.


" Majeshi ya waasi  yameondoka katika mji na majeshi ya serikali yameuchukua tena na kuanza operesheni ya kukamata watu nyumba kwa nyumba" alisema Mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la Kamal kutoka Ghouta huko Damascus.
.
Muongeaji wa kikundi cha waasi cha FSA, Mahel al-Naimi pia amethibitisha habari hizo na kusema majeshi ya Syria yameingia na kuchukua vitongoji hivyo ingawa wao bado wapo karibu na mji huo.
Wanaharakati walisema kiasi cha Vifaru 50 na magari mengine ya kivita yaliingia katika vitongoji hivyo hapo jana ambapo raia 19 na waasi waliuawa. Mmoja wa mashuhuda mjini humo Bw. Kfar Batna aliita vita hiyo kuwa "Vita ya mjini" na kueleza kuwa Miili mingi ya watu waliokufa  imetapakaa katika mitaa ya mji huo.

Waasi hao walikua wameshikilia baadhi ya vitongoji vilivyo umbali wa kilometa 8 kutoka kati kati ya Mji mkuu wa Damascus.

Mfululizo wa vitendo vya umwagaji damu na vurugu mjini Syria vinazidi kuongezeka  hali ilyowafanya waangalizi wa Umoja wa nchi za kiarabu kuondoka nchini humo ambapo umoja huo ambao unataka rais Al Asad ajiuzuru umepanga kufanya mkutano wake Februari 5 kujadili hatima ya Nchi hiyo.Umoja wa mataifa Pia umekuwa katika juhudi za kumaliza machafuko hayo ingawa wanchama wake China na Russia wenye Kura za Veto wameonekana kulega kuunga mkono azimio la kuchukuliwa hatua dhidi ya Serikali ya Syria.

Friday, January 27, 2012

UHURU KENYATA AJIUZURU KENYA

NAIROBI, 
Kenyan Finance Minister Uhuru Kenyatta in a file photo. President Mwai Kibaki has accepted the resignation of  Kenyatta, the presidential spokesman said on Thursday.  REUTERS/Thomas Mukoya
- Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Uhuru Kenyatta amejiuzulu leo siku chache baada ya jina lake kuonekana katika watuhumiwa wa uchochezi wa fujo za uchaguzi wa mwaka 2007 iliyotolewa na mahakama ya kimataifaa ya makosa ya jinai (ICC) hivi karibuni.
           Hata hivyo katika kuonesha kuwa huo sio mwisho wa harakati zake katika siasa Kenyatta amehusishwa nu kugombea urais mwaka 2013 safari hii akiungana na aliyekuwa adui yake katika fujo na uchaguzi wa mwaka 2007 ndugu William Ruto ambaye pia ni mtuhumiwa wa ICC katika fujo hizo za uchaguzi wa mwaka 2007. Kenyatta na Ruto wanadaiwa kuchochea makundi ya vijana kutoka katika itikadi, makbila  na sehemu tofauti  kupigana na kuuana punde baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya mnamo mwaka 2007 kumalizika.
[-] Text [+]

           Kenyatta mwenye miaka 50 mtoto wa Jomo Kenyatta baba wa taifa la Kenya na tajiri zaidi Nchini Kenya alikuwa akipata shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa wabunge wenzake kufuatia kupatikana na kesi ya kujibu na mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai.
           Ni desturi nchini Kenya kwa mawaziri wanaotuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma kujiuzulu ingawa Mwanasheria mkuu wa Kenya Kenyatta and Muthaura wangeweza kuendelea na nafasi zao mpaka hapo rufaa walizokata kwa mahakama hiyo ya kimataifa kukataliwa suala ambalo huchukua hadi mwaka mmoja.

Thursday, January 26, 2012

MAKAMU JAJI MKUU KENYA ASIMAMISHWA KAZI.1/

NAIROBI, KENYA.
        Rais wa Kenya Mh.Mwai Kibaki amemsimamisha kazi makamu jaji mkuu wa nchi hiyo bi. Nancy Baraza kufuatia tuhuma za kutishia maisha kwa kutumia silaha zinazomkabili na kuunda jopo maalum la kumchunguza.
         Bi.Baraza anatuhumiwa kumtishia kwa bastola mlinzi wa duka moja bi. Rebbecca Kerubo siku ya mkesha wa mwaka mpya kufuatia kukosekana kwa maelewano kati yao.Taaria kutoka ikulu imesema Bi.Baraza hatoendelea na majukumu yake ya kimahakama mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na kkuonekana hana tuhuma, ambapo kwa wakati huu aliosimamishwa atakuwa akilipwa nusu mshahara.
Taarifa hiyo imemtaja Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania Bw.Augustino Ramadhan kama mwenyekiti wa Jopo hilo na  wengine ni Prof Judith Behemuka, Philip Ransley, Surinder Kapila, Beuttah Siganga, Grace Madoka na Prof Mugambi Kanyua wenye nafasi kama wajumbe.