Sunday, March 30, 2014

Urais wamponza Sitta

 Samuel Sitta avuruga kanuni kutaka urais 2015

MWENENDO wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, umeanza kutiliwa shaka huku baadhi ya wajumbe wenzake wakidai anateswa na dhambi ya unafiki.
Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano kwa uwezo mkubwa chini ya falsafa yake ya viwango na kasi, alichaguliwa kwa kura nyingi kuongoza Bunge la Katiba akiahidi kuendeleza falsafa hiyo.
Hata hivyo Sitta ameanza kushindwa kuitekeleza ahadi hiyo baada ya kuruhusu kufinyangwa kwa kanuni za Bunge pamoja na kufanya uteuzi wa wajumbe wa kamati ya uongozi akiwapendelea wajumbe kutoka CCM.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa kuyumba huko kwa Sitta kunachangiwa na ndoto zake za kutaka kuwania urais mwaka 2015, hivyo anatafuta kuungwa mkono na CCM.
Sitta anatafuta kuungwa mkono na CCM kwakuwa chama hicho mwaka 2010 mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu kilimtosa kuwania uspika kwa madai ni zamu ya mwanamke.
Miongoni mwa sababu zilizokuwa zikitajwa chinichini ni kuwa kiongozi huyo wakati akiwa spika aliruhusu mijadala iliyozusha makundi ndani ya chama na serikali.
Katika utawala wake Sitta, aliunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza zabuni iliyoipa ushindi wa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond, iliyokuwa ikilipwa sh milioni 152 kwa siku.
Kamati teule hiyo iliyokuwa chini ya Dk. Harrison Mwakyembe, ilitoa ripoti iliyobaini kulikuwa na utata katika kuipa ushindi zabuni ya Richmond, waliodai ni ‘hewa’ na yenye mkono wa ‘bwana mkubwa’.
Kashafa hiyo ilimfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu baada ya kuguswa na kashfa hiyo.
Hata hivyo mchakato huo ulifungwa na Sitta, katika mazingira ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), aliyeguswa pia na kashfa hiyo akitaka iundwe tume huru ya majaji watatu kuchunguza sakata hilo.
Tangu hapo Sitta, amekuwa kwenye uahasama mkubwa na makada wenzake pamoja na chama ambacho kinaamini utawala wake ndio uliozalisha wapinzani wengi bungeni hivi sasa.
Kutokana na dhana hiyo, Sitta hivi sasa amekuwa akifanya mambo yanayoonekana kutafuta huruma ya chama chake ambapo pia nusuru kisimpe ridhaa ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, nafasi iliyokuwa ikitajwa kukaliwa na Andrew Chenge.
Miongoni mwa mambo anayoshutumiwa kuyafanya Sitta ni kuwakemea wenzake kwa ufisadi wanaoufanya wanapotoa fedha kwenye harambee na shughuli za kijamii ilhali naye amekuwa akipita makanisani kuomba huruma ya wananchi.
Sitta pia analaumiwa kwa kuruhusu uvunjwaji wa kanuni za kuliongoza Bunge kwa kuruhusu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe rasimu ya katiba kabla ya Rais Jakaya Kikwete.
Inadaiwa alifanya hivyo ili kumtengenezea mazingira Rais Kikwete, kujibu mapendekezo yaliyokuwamo kwenye Rasimu ya Katiba ili kuipa ahueni CCM inayopinga mfumo wa serikali tatu uliopendekezwa kwenye rasimu.
Sitta pia anadaiwa kufanya uteuzi wa wajumbe watatu kati ya watano kuingia katika kamati ya uongozi ambayo inaongozwa na wenyeviti 12 kutoka CCM.
Miongoni mwa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ni Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikataa uteuzi huo huku akimlaumu Sitta kwa kufanya uteuzi unaoangalia zaidi masilahi ya chama chake kuliko taifa.
Baadhi ya wajumbe hususan wapinzani wanadai Sitta anayumbishwa na Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), hivyo kufikia hatua ya kuzivunja kanuni za Bunge na kuibua mivutano.
Udhaifu wa Sitta
Baadhi ya wajumbe wa upinzani wanasema tabia ya kutokuwa na msimamo aliyoanza kuionyesha Sitta hivi sasa kwa kufuata matakwa ya chama chake bila kujali uzito wa hoja husika kumemvunjia heshima.
Hoja yao ni kuwa falsafa ya ‘Kasi na Viwango’ aliyoitangaza ameshindwa kuionyesha katika Bunge Maalumu kiasi cha kuyumbisha mchakato wa mijadala bungeni.
Pia ndani ya CCM, Sitta anatazamika kwa sura mbili. Mosi, washindani wake kisiasa wanadai anaongoza Bunge hilo kwa kuwasikiliza zaidi wapinzani ili kujijengea uhalali wa kugombea urais 2015.
Kundi la wafuasi wake, lenyewe linaona kama Sitta yuko imara kusimamia mchakato wa Katiba isipokuwa anakwazwa na mahasimu wake ndani ya chama wanaomuundia zengwe aonekane dhaifu.
Kangi Lugola (CCM), alikuwa wa kwanza kumtahadharisha Sitta kuhusiana na uongozi wake, akisema nafasi yake ni sawa na Jaji wa Mahakama Kuu aliyepelekewa mtuhumiwa wa mauaji amhukumu.
“Sitta ndiye amepewa jukumu la kuhakikisha anasimamia mchakato huu ili wananchi wapate Katiba mpya na nzuri, kushindwa kufanya hivyo wananchi wataondoa imani kwake na chama,” alisema Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Mwibara.
Lugola aliongeza kwamba licha ya CCM kuwa na wajumbe wengi katika Bunge hilo lakini Sitta alichaguliwa kwa kuaminiwa kutokana na utashi wake wa kisiasa, hivyo anapaswa kutumia busara.
Naye Godbless Lema (CHADEMA) alimtaka Sitta kuwa makini na kila iana ya ushauri anaopewa na wenzake ndani ya CCM, kwamba mwingine una lengo la kumchafulia rekodi yake.
Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, alisema kuwa wabaya wa Sitta wamekuwa wakijidai kumshauri hata mambo ambayo baadaye yanaleta matatizo kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa alishindwa kusimamia mchakato wa kuandika katiba.
“Wako wabaya wako wanataka mchakato huo usifanikiwe ili ionekane ulishindwa kusimamia wananchi wapate katiba, hivyo waseme haufai hata kugombea urais,” alisema Lema bungeni.
Naye  John Shibuda, anasema Sitta anatafunwa na dhambi ya unafiki wake ambao hauwezi kumfikisha katika anachokifikiria.
Shibuda alisema Sitta amejikuta wakati mwingine akifanya uamuzi wa kuibeba CCM ili kujinafikisha aonekane ni kada mwaminifu na wakati huo huo anataka kujijengea ushujaa ili katiba mpya ipatikane, atumie turufu hiyo kujipigia debe la urais 2015.
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema Sitta ni dhaifu na ndiyo maana anashindwa kuongoza Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu ya kuegemea zaidi kwenye chama chake.
Dk. Slaa alisema uongozi wa Sitta bungeni utasababisha mivurugano mikubwa na kutoelewana baina ya wajumbe waliopewa jukumu la kuandika Katiba inayopendekezwa, ambayo itakwenda kupigiwa kura ya maoni na wananchi.

Sitta amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wajumbe tangu siku ya kwanza alipokalia kiti hicho kuwa anavunja kanuni alizotamba kuzisimamia kwa kasi na viwango.

Wednesday, March 19, 2014

WARIOBA ATEGUA KITENDAWILI SERIKALI TATU.


Dodoma/Dar. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba jana aliliteka Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, alipowasilisha Rasimu ya Katiba na kushangiliwa katika maeneo mengi nyeti na kupigiwa kelele katika vipengele vichache vya uraia na ardhi.
Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu – Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema Warioba katika hotuba yake ya aya 191 ambayo imechapwa kwa ukamilifu ndani ya gazeti hili.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji Warioba alisema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.
“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba.  Waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,” alisema.
Alisema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya Tanzania Bara tu.
“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,” alisema. 
Warioba alishangiliwa tena na baadhi ya wajumbe aliposema: “Muundo wa Serikali Tatu haupunguzi uimara wa Muungano na muungano huo ni wa nchi mbili kwa manufaa ya wananchi, “Faida kubwa iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita ni kuungana kwa wananchi.”

Saturday, March 15, 2014

MACHAFUKO BRAZIL YAITOA KIJASHO FIFA

MO FAHAH ATETEA UAMUZI WAKE

VIONGOZI WA YANGA WAONYESHA MFANO WA KUIGWA KWENYE MATUMIZI YA FEDHA ZA KLABU


Uongozi wa klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans umeonyesha mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa soka nchini siku moja baada ya kurudi kutoka Misri walipoenda na timu kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya  klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.

"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.

VAN PERSIE: NINA FURAHA MAN UNITED, NA NINATAKA KUENDELEA KUWA HAPA HATA BAADA YA MKATABA KUISHA."


Mshambuliaji Manchester United Robin van Persie amesema rasmi kwamba anataka kubakia Old Trafford kwa muda mrefu. 
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 30 amekanusha kwamba haelewani na kocha David Moyes na imekuwa ikisemekana kwamba angeondoka kwenye timu hiyo kipindi kijacho cha usajili.  
Lakini nahodha wa Uholanzi anasisitiza kwamba anapendelea kubakia United.
"Ukweli ni kwamba nina furaha sana," Alisema. "Nilisaini mkataba wa miaka minne na nina furaha kuendelea kukaa hapa kwa muda mrefu, hata baada ya miaka yangu miwili iliyobaki." 
Pia tetesi zimekuwa zikisema kwamba Van Persie havutiwi na mbinu za ufundishaji za Moyes. 
Lakini akiongea katika interview aliyofanyiwa na United Review, kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Liverpool, aliongelea juu ya saula la mbinu za Moyes. 
"Hakuna shaka kwamba ninajifunza mbinu mpya na ninaendelea vizuri chini ya David Moyes," alisema. "Vipindi vya mazoezi tunavyokuwa kuwa navyo ni vizuri mno na ninajifunza vitu vingi kutoka kwenye mazoezi hayo kila siku. 
"Kuna hali nzuri ya kuheshimiana baina yetu na mazingira yetu ya kufanya kazi ni mazuri. Moyes anataka sana kazi iende vizuri na mie ninataka hivyo pia."

VAN PERSIE: NINA FURAHA MAN UNITED, NA NINATAKA KUENDELEA KUWA HAPA HATA BAADA YA MKATABA KUISHA."


Mshambuliaji Manchester United Robin van Persie amesema rasmi kwamba anataka kubakia Old Trafford kwa muda mrefu. 
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 30 amekanusha kwamba haelewani na kocha David Moyes na imekuwa ikisemekana kwamba angeondoka kwenye timu hiyo kipindi kijacho cha usajili.  
Lakini nahodha wa Uholanzi anasisitiza kwamba anapendelea kubakia United.
"Ukweli ni kwamba nina furaha sana," Alisema. "Nilisaini mkataba wa miaka minne na nina furaha kuendelea kukaa hapa kwa muda mrefu, hata baada ya miaka yangu miwili iliyobaki." 
Pia tetesi zimekuwa zikisema kwamba Van Persie havutiwi na mbinu za ufundishaji za Moyes. 
Lakini akiongea katika interview aliyofanyiwa na United Review, kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Liverpool, aliongelea juu ya saula la mbinu za Moyes. 
"Hakuna shaka kwamba ninajifunza mbinu mpya na ninaendelea vizuri chini ya David Moyes," alisema. "Vipindi vya mazoezi tunavyokuwa kuwa navyo ni vizuri mno na ninajifunza vitu vingi kutoka kwenye mazoezi hayo kila siku. 
"Kuna hali nzuri ya kuheshimiana baina yetu na mazingira yetu ya kufanya kazi ni mazuri. Moyes anataka sana kazi iende vizuri na mie ninataka hivyo pia."

KINANA: NAWAJUA WASALITI KUMI CCM.

Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana na miongozo ya chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao haizidi kumi. Kauli hiyo ya Kinana inafuatia taarifa zilizoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kuwa, CCM kimeanza kuwahoji baadhi ya wabunge wake, ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu ya kupingana na maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo wa Serikali mbili. “Sisi (CCM) hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na msimamo tofauti, kwani hawa wenye msimamo tofauti na chama hawazidi kumi ama siyo zaidi ya 15,” alisema Kinana na kuongeza; “Hawa watu mimi nawajua kwa majina, mmoja (jina tunalo) ni hatari zaidi kwa sababu anaweza kuwakusanya wengine na kuwashawishi wafuate msimamo wake, lakini waliobaki wote, hawatishi kwa kuwa wanabaki na misimamo yao wenyewe.” Kwa mujibu wa habari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni wale wanaotokana na Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na ambao wanataka Muundo wa Serikali tatu. “Ni kweli hata mimi niliitwa na akaniambia (mwakilishi wa chama) ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha ya watu 90 na nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,” alieleza mmoja wa wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Maelezo ya Kinana Kinana aliliambia gazeti hili kuwa, kulingana na muundo wa chama hicho tawala, viongozi wanaoweza kuwahoji watu ni yeye Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa chama Taifa. “Tena tunafanya hivyo kwenye vikao maalumu na kwa sababu ambazo haziwezi kuwa siri.” Kinana alieleza kuwa taarifa kwamba CCM imewahoji watu 90 kutokana na kuwa na misimamo tofauti na chama hicho kuhusu Serikali mbili na kura ya wazi, siyo za kweli na anaamini imesambazwa na watu kwa malengo yao binafsi. Kinana anafafanua kuwa CCM kama chama kikubwa nchini chenye wafuasi karibu nchi nzima, hakiwezi kudhibiti mitizamo ya watu na kimsingi tofauti za mitazamo ndiyo msingi wa demokrasia. Novemba 20 mwaka 2012 akizungumza katika kipindi cha Jenerali on Monday kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Kinana alitoa onyo kwa makada wasaliti kuwa atasimamia utekelezaji wa uamuzi wa Halmashuari Kuu ya CCM (Nec) ya kuwabaini na kuwaondoa viongozi wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama na kukipaka matope. Kura ya wazi na Serikali mbili Katika hatua nyingine, Kinana alizungumzia msimamo wa chama hicho wa kura ya siri na muundo wa Serikali mbili, akieleza kuwa siyo jambo la ajabu, kwani katika mchakato wa kutunga katiba, kila kundi lina maoni na mtazamo wake na kuutetea kwenye mijadala. “Wanaosema kuna vyama havina msimamo pale bungeni ni waongo. Siyo vyama tu, kila kikundi kina msimamo unaotokana na uchambuzi wao wa hali ya siasa nchini na wanachofikiri kina masilahi kwa nchi na watu wanaofuata mtazamo wao. Hawawezi kuniambia kama Lipumba (Profesa Ibrahim) na Mbowe (Freeman), hawana wanachosimamia kwenye mjadala huo wa Bunge Maalumu,” alisema

Friday, March 14, 2014

SITTA:KURA YA SIRI

 

Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amezungumzia uwezekano wa kutumia kura ya siri katika kuamua ibara nyeti katika Rasimu ya Katiba. Sitta aliyechaguliwa juzi kushika wadhifa huo, alisema atashirikiana na kamati ya uongozi itakayoundwa ya wenyeviti wa Kamati 15 za Bunge hilo na kamati ya ushauriano kupata jawabu la suala hilo. - See more at: http://bungelakatiba.blogspot.com/2014/03/samuel-sitta-kura-ya-siri.html#sthash.XysswCrd.dpuf Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, Sitta alisema: “Unajua kuna baadhi ya vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba ni vizuri vipigiwe kura ya wazi na vingine ambavyo ni nyeti zaidi vipigiwe kura ya siri.” Alisema si vizuri vifungu vyote vipigiwe kura sawa, yaani si lazima zote ziwe za siri au ziwe za wazi. Alitoa mfano wa ibara inayosema kutakuwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na kusema: “Hatuwezi kushindana katika suala la kuwapo kwa Mahakama na ni wazi kuwa jambo hilo mnaweza kupiga kura ya wazi. Nasema hivyo kwa sababu Katiba yoyote lazima ionyeshe mihimili yote ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama.” Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alishinda kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika juzi kwa kura 487 kati ya 563 (sawa na asilimia 85). Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye kaulimbiu yake ni ‘kasi na viwango’, alisema vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba vinavyoweka misingi ya Katiba, ni vizuri vikapigiwa kura ya siri. - See more at: http://bungelakatiba.blogspot.com/2014/03/samuel-sitta-kura-ya-siri.html#sthash.XysswCrd.dpuf

RWANDA 'VITANI' NA AFRIKA KUSINI-YAJIBU MAPIGO KUVUNJA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA.

 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ,Bi Louise Mushikiwabo, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ameeleza kwamba Rwanda ilikuwa na haki zote kuwafukuza mabalozi wa Afrika Kusini mjini Kigali ikizingatia hatua ambayo nchi hiyo ilianzisha yenyewe kwa kuwatimua maafisa wa ubalozi wa Rwanda mjini Johannesburg.
Katika ujumbe wake mfupi kwenye mtandao huo Bi Mushikiwabo, anailaumu Serikali ya Afrika Kusini kwa kutochukua hatua dhidi ya wanyarwanda waliokimbilia nchini humo ambao serikali ya Rwanda inawatuhumu kuendelea na hujuma za kigaidi dhidi ya Rwanda na kwamba Pretoria haijatekeleza muafaka uliofikiwa awali.
Kulingana na kiongozi huyo kupitia mtandao wa twitter, mahusiano mema kati ya Rwanda na Afrika Kusini yatafikiwa wakati suala la kisheria kuhusu wanyarwanda waliokimbilia nchini humo itapata ufumbuzi.
Wakati haya yakiarifiwa ,mjumbe maalum wa Rais Baracka Obama wa Marekani katika mataifa ya ukanda wa maziwa makuu, Russ Feingold,alisema kuwa Marekani inafuatilia kwa karibu mzozo huo ambao alielezea waandishi kwamba mataifa ya Rwanda na Afrika ya kusini hayana budi kumaliza tofauti zao kwa njia ya kidiplomasia.
Mjumbe huyo alikutana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukutana na Rais Paul Kagame.
Miongoni mwa wanyarwanda waliokimbilia Afrika ya kusini ni Generali Kayumba Nyamwasa ambaye amekuwa akilaumu utawala wa Rwanda kwa kuhusika na mashambulizi kadhaa dhidi yake ambayo amenusurika.
Kwa upande mwingine Serikali ya Rwanda inakanusha vikali kuhusika na tuhuma hizo.
Kayumba Nyamwasa anajulikana kama mtu aliyetangaza wazi kupiga vita utawala wa Rwanda na anatuhumiwa kuhusika katika mashambulizi ya hapa na pale yanayogharimu maisha ya watu na mali.

Monday, March 10, 2014

Obama amualika Waziri Mkuu wa Ukraine

Rais wa Marekani Barrack Obama, amemualika waziri mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk, mjini Washington kwa mashauriano kuhusiana na mzozo unaokumba taifa lake.
Ikulu ya White House, imesema kuwa mkutano huo utakaofanyika siku ya Jumatano, utaangazia, mbinu za kutafuta suluhisho la amani, kuhusiana na operesheni za kijeshi zinazoendesha na jeshi la Urussi katika eneo la Crimea.
Waandishi wa habari wanasema kuwa mualiko huo ni ni ishara thabiti kuwa Marekani inaunga mkono utawala wa mpito wa Kiev.
Wakati huo huo, jamii ya kimataifa inaendelea kuishinikiza utawala wa Moscow, kuondoa wanajeshi wake katika eneo la Crimea.
Chansella wa Ujerumani, Angela Merkel, amemueleza rais wa Urussi, Vladimir Putin, kutilia maanani kuwa kura ya maoni kuhusu ikiwa eneo hilo la Crimea, litajiunga na Urussi inakiuka sheria na ni haramu.


Rais Obama
Huku hayo yakijiri, mfungwa wa zamani na mfanya biashara maarufu wa secta ya mafuta na mkoasoaji mkubwa wa rais Putin, Mikhail Khodorkovsky, anehutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika mji mkuu wa Ukraine Kiev.
Amewaambia maelfu ya watu waliofurika katika medani ya Uhuru kuwa serikali ya Urussi inawahadaa raia wake kwa kuwahusisha waandamanaji mjini Kiew na watu wanaopinga utawala wake na raia wake.
Mikutano kama hiyo imefanyika katika sehemu kadhaa za nchi hiyo.
Nyingi zikiwa za amani lakini mjini Sevastopol, katika eneo la Crimea, raia wa Ukraine wanaozungumza lugha ya Kirussi waliwapiga watu wanaounga mkono serikali ya Ukraine.
Televisheni zilizo na makao yao mjini Kiev zimezuiliwa kurusha matangazo katika eneo hilo la Crimea.

Orodha ya Wanasoka 10 tajiri duniani, etoo' no.3.

Ni miongoni mwa zile stori ambazo mashabiki wengi hupenda kuzifahamu au hata kuziongelea kwenye vijiwe mbalimbali lakini uhakika umetolewa na mtandao unaodili na stori za soka kwa sana.
Katika listi hiyo iliyotajwa leo, Ronaldo amemrithi David Beckham ambaye alistaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita ambapo Ronaldo ana utajiri wa paundi millioni 122.
Lionel Messi ameshika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa paundi millioni 120, nafasi ya tatu imekamatwa na muafrika pekee kwenye listi hii ambae ni Samuel Etoo mwenye utajiri wa paundi millioni 70, Rooney anafatia kwa utajiri wa paundi millioni 69 huku Kaka akishika nafasi ya 5 kwa utajiri wa paundi millioni 67.
Listi inaendelea kama ifuatavyo
players copy

Chanzo:millardayo.com













Saturday, March 8, 2014

CHELSEA WASHINDA 4-0 DEMBA BA APIGA 2.

View image on Twitter 
Timu ya Chelsea imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuwatungua Totenham kwa mabao 4-0, mabao yakifungwa na Etoo dk.56, Hazard dk  60, Demba Ba dk.88 & 90.


Referee: Michael Oliver
Lineups
Chelsea: Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Ramires, Matic, Lampard; Schurrle, Hazard; Eto'o/Demba Ba.

Tottenham Hotspur: Lloris; Naughton, Dawson, Kaboul, Vertonghen; Bentaleb, Sandro; Walker, Lennon, Sigurdsson; Adebayor

Ndege ya Malaysia yapotea na abiria 239

 
Juhudi za kimataifa zinaendelea kutafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia iyokuwa ikielekea Beijing nchini China na kupotea baharini ikiwa na abiria 239. Ndege hiyo iliyopotea aina Boeing 777 ilkuwa na abiria wapatao 239 pamoja na wafanyakazi wa ndege. Asia ya Kusini Mashariki imeongeza nguvu katika juhudi hizo za kutafuta ndege hiyo iliyopotelea katika eno la bahari la Malaysia na Vietnam . Shirika la ndege la Malaysia limesema ndege hiyo namba MN370 ilipotea majira ya saa 8:40 kwa saa Malaysia siku ya Ijumaa baada ya kuondoa Kuala Lumpur. Jeshi la Malaysia limesema kikosi cha pili cha helikopta na Meli kimetumwa kwenye eneo la tukio lakini hata hivyo hakuna chochote kilichoonekana katika hatua za awali za utafutaji wa ndege hiyo. Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili Beijing China majira ya saa 12:30 kwa saa za Malaysia. Waziri wa Usafiri wa Malaysia amesema hakuna taarifa za zozote za kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo. "Tunafanya kila linalowezekana ndani ya uwezo wetu kujua ndege hiyo ilipo," Hishammuddin Hussein amewaambia waandishi wa habari katika mji Kuala Lumpur. 

Chanzo:BBC Swahili.

Wednesday, March 5, 2014

Sitta afanya mazoezi kuongoza Bunge

Dodoma. Siku moja baada ya kuteuliwa na CCM kuwania uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema ameanza kupitia sheria na kanuni zitakazomwezesha kuliongoza huku akiahidi kutenda haki kwa wajumbe wote iwapo atachaguliwa.
Akizungumza mjini Dodoma jana, Sitta alisema: “Nawashukuru wote waliokuwa wakiniunga mkono na niseme wazi kuwa nitatenda haki kwa wajumbe wote wa Bunge Maalumu la Katiba.”
Alisema kazi kubwa aliyonayo baada ya uteuzi huo ni kuhakikisha kuwa anazipitia sheria na kanuni zinazoongoza bunge hilo na sheria nyingine kwa kuwa ndizo nyenzo zake za utendaji kazi.
Akizungumzia mchakato wa uteuzi ndani ya chama hicho na mchuano uliokuwapo kati yake na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge alisema: “Hii ni hatua ya awali na ya kawaida tu ndani ya CCM. Mara nyingi chama changu kikiona kuna mambo yanayoleta msuguano, basi huamua kuteua jina moja kwa ajili ya kugombea. Wameteua majina mawili kwa demokrasia kabisa. Ninakishukuru chama changu kwa kuniteua na kwa sasa najiandaa na uchaguzi.”
Suluhu: Nitafanya maajabu
Kwa upande wake, Mjumbe wa bunge hilo aliyeteuliwa na CCM kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba ana uwezo mkubwa wa kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba na hana shaka katika uteuzi wake.
Samia ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), alijisifu akisema ana rekodi nzuri ambayo haitiliwi shaka kwa weledi wake na haoni tatizo kwa yeye kupewa nafasi hiyo.
“Nina rekodi nzuri ya kuongoza Serikali kwa muda mrefu na sijapata doa lolote, kwa hiyo sioni ugumu wowote,” alisema.
Samia aliwahi pia kuwa Waziri wa Ajira na Wanawake na baadaye, Waziri wa Utalii katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kuwa Waziri wa Nchi, katika Ofisi ya Makamu wa Rais.
Kinana na mchakato
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alizungumzia mchakato uliompitisha Sitta kuwania nafasi hiyo na kusema ulilenga kuzuia mgawanyiko ndani ya chama.
Hata hivyo, alisema Chenge aliamua kwa hiari yake kujitoa baada ya kukubaliana na Sitta walipoitwa na uongozi wa chama kwa ushauri. Akizungumza katika mahojiano maalumu mjini Dodoma, Kinana alisema: “Kiutaratibu, yeyote ilimradi awe mjumbe wa Bunge la Katiba, angeweza kujitokeza kugombea uenyekiti. CCM, walijitokeza wawili walionyesha nia; Sitta na Chenge.

Tuesday, March 4, 2014

Luis Suarez asaini mkataba mpya


 
Everton ikiwa mbele ya Chelsea, katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza, baada ya kuifunga Swansea mabao (2-1), na kuipa shinikizo the Bleus ambayo itakwaruzana na Arsenal leo jumatatu. Tottehnam imefungwa na Southampton mabao (3-2).
Chelsea ambayo ilishapoteza mara moja msimu huu, imekua na shauku toka tarehe 5 mwezi oktoba kusogea mbele ikitoka kwenye nafasi ya 4. Chelsea ina alama 34, ikiwa mbele ya Arsenal alama 1.
Liverpool kwa sasa ndio inaongoza.



Hata hivo, Mshambuliaji mahiri wa Klabu ya Liverpoool Luis Suarez amesaini mkataba kuendelea kusakata gozi kwenye Klabu hiyo ya Liverpool.

Awali mkataba wa Suarez ambaye alijiunga na klabu hiyo January 2011 na akiwa tayari amekwishafunga mabao 17 msimu huu, ulitaraji kukamilika mwaka 2016.

Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 26, amesema amefurahi kufikia makubaliano ya kuendelea kuitumikia kwa muda mrefu klabu hii ya Liverpool, akibaini kwamba timu hio ina wachezaji mahiri, na inazidi kuimarika kila wakati.

Naye kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa hiyo ni habari njema kwa kila mdau wa Klabu ya Liverpool, wakiwemo wamiliki wa klabu lakini muhimu Zaidi Mashabiki wa klabu hiyo.

“Suarez ni mchezaji wa kiwango cha dunia, mwenye kipaji cha hali ya juu, na kwa kuendelea kuwa naye wakati huu ni jambo la msingi katika kile tunacholenga kukipata hapa klabuni kwetu”, amesema Brendan.

Kocha huyo wa Liverpool amesema wtaendelea kushuhudia ubora wa Luis Suarez siku zijazo,akiwa ndani ya jezi za Liverpool.

Kesi ya mauaji ya bingwa wa mbio za paralympic Oscar Pistorus inaendelea

Оскар Писториус в зале суда в Претории 03/03/2014

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mwenye ulemavu wa Miguu Oscar Pistorius raia wa Afrika Kusini, hii leo imeingia siku yake ya pili kwa upande wa utetezi kuwahoji mashahidi wa Serikali.

Hii leo shahidi wa pili kwenye kesi hiyo ambaye ni jirani wa Oscar Pistorius ameieleza mahakama namna alivyosikia milio ya risasi na kelele za kuomba msaada toka kwa mpenzi wa Pistorius na kwamba jambo hilo lilimfanya ahisi kulikuwa na ujambazi kwa jirani yake.
Lakini wakati shahidi huyu wapili akieleza kile alichokisikia, hapo jana shahidi wa kwanza kwenye kesi hiyo alijikuta matatani wakati akihojiwa na upande wa utetezi kutokana na kutofautiana kwa kauli zake na hata wakati fulani kuangua kilio kilichopuuzwa na mawakili wa Pistorius.
Katika hatua nyingine jaji anayesikiliza kesi hiyo, Thokozile Masipa amevionya vyombo vya habari dhidi ya kuchapisha picha za mashahidi ambao wamekataa sura zao kuoneshwa hadharani na kwamba atavichukulia hatua vyomb vyote vya habari vitakavyokiuka amri ya mahakama.
Hapo jana kituo kimoja cha televisheni nchini humo kilionesha picha ya shahidi ambaye ni mhadhiri wa chuo kimoja mjini Pretoria wakati akihojiwa na upande wa utetezi hali iliyoamsha toka kwa wanaharakati.

Urusi yaionya Marekani dhidi ya vitisho

mkutano wa vyombo vya habari wa rais wa Urusi Vladimir Poutine, March 4, 2014 jijini Moscou

Nchi ya Urusi imeionya serikali ya Marekani dhidi ya hatua yoyote iliyopanga kuchukua ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuongeza kuwa atakaeumia kwenye mzozo huo atakuwa ni Marekani mwenyewe. Kauli ya Urusi inatolewa wakati huu ambapo rais wa Marekani Barack Obama akitishia kusitisha ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Urusi ambapo pia amesharangaza kusitisha ushirikiano wa kijeshi na taifa hilo kufuatia hatua yake ya kuivamia nchi ya Ukraine. Urusi inasisitiza kuwa inauwezo wa kusimama yenyewe hata bila ya kutegemea wafanyabiashara toka nchini Marekani.



TWaziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amewasili nchini Ukraine jumanne hii ambapo atakuwa na mazungumzo na utawala wa mpito wa taifa hilo ambao wameomba msaada toka jumuiya ya kimataifa.
Ziara ya Kerry inafuatia ziara kama hiyo ambayo imefanywa hapo jana na waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague ambao wote kwa pamoja wanalenga kusisitiza kutoridhishwa kwao na namna ambavyo Urusi imeivamia kijeshi nchi ya Ukraine.
Tayari waziri mkuu mpya wa Ukraine, Arseni Iatsenuik ametoa matamshi mengine kukashifu utawala wa Urusi na kuionya kuhusu kuendelea kusonga mbele kwa vikosi vyake kwenye mji wa Crimea.
Kauli ya Arseni iliungwa mkono na waziri mkuu wa Uingereza David cameron ambaye amesisitiza kuwa nchi yake itachukua hatua kali dhidi ya Urusi iwapo itaendelea kuingilia uhuru wa taifa hilo.
Awali wakati wa kikao cha tatu cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Urusi Vitaly Churkin alitetea uamuzi wa nchi yake kupeleka wanajeshi kwa kile alichodai waliombwa kufanya hivyo na rais aliyeoondolewa madarakni Viktor Yanukovich.
Kauli ya Churkin inakosolewa vikali na balozi wa Marekani kwenye umoja huo, Samantha Power ambaye amekiita kitendo cha urusi kama ni chakutaka kuhalalisha jambo haramu.

Katika hatua nyingine rais Vladmir Putin kwa mara ya kwanza amezungumza na wanahabari na kusisitiza kuwa wanajeshi wake hawakushiriki oporesheni zozote za kuteka bunge la Crimea wala kuwaweka mateka wanajeshi wa Ukraine.

Serikali ya Burundi yakanusha tuhuma za kuhujumu vyama vya upinzani

Willy Nyamitwe, naibu msemaji wa rais wa Burundi akiwa katika studio za RFI jijini Paris

Serikali ya Burundi imekanusha tuhuma za kuingilia shughuli za vyama vya upinzani kwa lengo la kuvidhoofisha kama inavyodaiwa na vyama hivyo. Charles Nditije anaye kubalika kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Uprona, amesema kuwa chama tawala kinahusika katika matukio mengi ya kuvigawa vyama vya kisiasa, kwa malengo ya kujizatiti katika uchaguzi ujao. Mwishoni mwa mwezi Januari, Waziri wa Mambo ya Ndani Edouard Nduwimana alibadili maamuzi na kutangaza kumtabuwa Bonaventure Niyoyankana ambaye aliondolewa kwenye uongozi kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Uprona Badala ya Charles Nditije. Hatuwa ambayo ililaaniwa vikali na wafuasi wa chama Uprona.

Hata hivyo aliyekuwa makam wa kwanza wa rais kutoka chama Uprona alifuta maamuzi hayo ya waziri wa mambo ya ndani na hatimaye kufutwa kazi na rais wa jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza, hatuwa ambayo ilichukuliwa kama hujuma dhidi ya chama hicho na njama za kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Utata uliopo ni mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo ambapo vyama vya upinzani vinakituhumu chama tawala cha Cndd-Fdd kuwa na dhamira ya kufanya mabadiliko ya katiba, ili kumpa nafasi rais wa sasa kuwania muhula mwingine watatu.
Hata hivyo chama tawala nchini burundi hakijabainisha nani ataye wania urais mwaka 2015, licha ya kuendelea kutetea kuwa rais Nkurunziza bado ananafasi ya kuwania urais, kwani alichaguliwa na wananchi kwa muhula mmoja na umebaki muhula mwingine wa kuchaguliwa na wananchi.
Wanasiasa nchini Burundi wamekuwa wakiweka wazi kuhusu katiba ya Burundi iliofikiwa jijini Arusha nchini Tanzania, inayo baini kuhusu uongozi, na ugavi wa madaraka kati ya watu wa makabila ya wahutu na watutsi.
Tayari Chama cha Uprona kinachatajwa kuwa na wafuasi wengi wa kabila la watutsi, kimesema inavyoelekea kwa sasa chama tawala kinataka kuvunja mkataba wa Arusha na kuwanyima nafasi Watutsi jambo ambali msemaji wa chama Uprona tawi la Charles Nditije, Bonaventure Gasutwa anasema ni hatari sana.
Akihojiwa jana jijini Paris na Idhaa ya Kifaransa ya RFI naibu msemaji wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe, amesema walichokifanya ni kurejesha taasisi tawala baada ya baadhi ya wafuasi wa chama Uprona kujiondowa, na wapo sahihi kwakuwa walifuata sheria.
Kuhusu swala la usawa wa kikabila katika taasisi za uongozi, Willy Nyamitwe amesema katika chama tawala cha Cndd-fdd kuna watutsi wengi kuzidi idadi ya waliomo katika chama Uprona, hivyo usawa bado waendelea kutekelezwa
Aidha kuhusu mjadala uliopo juu ya rais wa sasa kuwania urais au la, Naibu msemaji wa rais Nkurunziza amesema baadhi wanaonakuwa rais Nkurunzia anaongoza muhula wa pili na wengine wanaonakuwa ni muhula wake wa kwanza ambapo alichaguliwa moja kwa moja na wananchi, na hapa ndipo mjadala unazunguukia, lakini ameendelea kusema huu mjadala haustahili kuwepo kwakuwa chama cha Cndd-fdd hakijafanya kongamano na kuamuwa nani atasimama kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho.

Mauaji zaidi yatokea Nigeria

Mkaazi wa kijiji cha Jakana karibu na mji wa Maiduguri jimbo la Borno amesema takriban watu 40 wameuawa katika shambulio lililofanywa na kundi la Boko Haram JUmatatu usiku.
Kaskazini mwa Nigeria imeshuhudia mashambulio ya kundi la Boko Haram licha ya operesheni ya jeshi inayoendelea.
Hapo Jumapili usiku watu 30 waliuawa katika shambulio mji wa Mafa na watu wengine 90 waliuawa katika siku ya Jumamosi katika shambulio la bomu mjini Maiduguri.
Chanzo:BBC SWAHILI.

Monday, March 3, 2014

URUSI YASIMAMIA HATUA ZAKE ZA KIJESHI UN.

Urusi imetetea uamuzi wake kutuma wanajeshi nchini Ukraine, katika kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa mataifa.
Balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa, Vitaliy Churkin, amesema kuwa rais wa Ukraine aliyeng'olewa madarakani Viktor Yanukovych alikuwa ameiomba Moscow kutuma wanajeshi ili kuwalinda raia na kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Akizungumza baada ya mkutano huo wa Baraza la Usalama, Balozi Vitaly Churkin amesema kuwa malalamishi ya bwana Yanukovich yanafanana na yale ya Urusi.
"Nadhani ni muhimu kuzingatia kwamba mtu tunayeamini kuwa ndiye rais halaIi wa Ukraine pia ana wasiwasi tulio nao kuhusu idadi kubwa ya raia wa Ukraine, kuhusu kinachoendelea. Na ametoa wito kwa Urusi kutumia majeshi yetu kuzuia mambo kuwa mabaya zaidi.''
Marekani imesitisha ushirikiano na Urusi.
Lakini balozi wa Ukraine, Yuriy Sergeyev, amesema kuwa madai ya Urusi hayahusiani na kile kinachojadiliwa kwani bwana Yanukovich hakuwa tena rais wa Ukraine.
"Hana lolote kwa sasa. Tukizungumzia hali ilivyo kwa sasa nchini Ukraine na madaraka ya kisheria ya mbunge ambalo lilimng'oa madarakani-hata balozi Churkin hivi leo kama ulisikia alichosema, ametaja kwamba tunaamini hatawahi kuwa rais wa Ukraine. Hii ina kwamba yeye siye mtu wa kuzungumza naye na hana lolote la kuzingatiwa."
Marekani imejibu kwa kusitisha mazungumzo ya kibiashara pamoja na uekezeji kati yake na Urusi, na idara ya Ulinzi ya Pentagon imetangaza kuwa ushirikiano wote wa kijeshi kati ya Marekani na Urusi ikiwemo mazoezi ya kijeshi, ziara za bandarini na mikutano ya mipango yote imesitishwa.

Mwelekeo mpya bungeni, Pinda atoa hoja .

Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanikiwa kutuliza hali ya hewa bungeni baada ya kutoa mapendekezo yaliyoungwa mkono na pande zote zilizokuwa zinavutana kuhusu kupitisha baadhi ya vifungu vya Kanuni za Bunge la Katiba.
Katika mapendekezo yake yaliyoungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Pinda alisema: “Nataka kuwaomba wenzangu wote kwenye maeneo hayo (yenye malumbano) tukiwa tunayapitia kama hatutaelewana tuyaache kwa muda na kumwomba Mwenyekiti aunde timu ya watu wazima na wenye busara wajaribu kuyatazama. “Tujadiliane, tushindane kwa lugha za staha, tusitumie lugha inayoweza kukasirisha. Isiwe mimi nimesema, mimi nimesema...”
Waziri Mkuu, aliwataka wajumbe wajiepushe na lugha za kuudhi ambazo zinaweza kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya.
Pinda alilazimika kuingilia kati baada ya kutokea mgawanyiko mkubwa wa namna ya kupiga kura kupitisha vifungu vya rasimu.
Akiunga mkono ushauri huo, Mbowe alisema Bunge limejaa hisia za hofu ndani na nje, jambo ambalo linatia wasiwasi wa kupatikana kwa Katiba Mpya. Alisema iwapo wajumbe watashirikiana na kuweka kando masilahi ya vyama, idadi yao katika makundi, Katiba inaweza kupatikana.
Vuai alionya kuhusu matumizi ya lugha za kuudhi huku Profesa Lipumba akiwataka wajumbe kuzingatia masilahi ya Taifa kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete na kutengeneza Katiba ya Watanzania wote bila ya kujali masilahi binafsi.
Upigaji kura bungeni vita
Awali, mjadala wa utaratibu wa upigaji kura katika Bunge hilo ulichukua sura mpya baada ya kudaiwa kuwapo ushawishi unaohusisha utoaji wa bahasha ili kutaka kuungwa mkono katika misimamo inayokinzana.
Habari zilizopatikana zilidai kuwa watuhumiwa katika sakata hilo ni baadhi ya wajumbe ambao ni mawaziri na mbunge mmoja wa CCM. Vigogo hao wanadaiwa kuwashawishi wajumbe ambao hawatokani na vyama vya siasa ili kupitisha agenda ya kura ya wazi kirahisi.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mjumbe wa Bunge hilo, Julius Mtatiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, alisema: “Jaribio la kuzuia kura ya siri limechukua njia za aibu, baada ya CCM kutumia fedha kushawishi wajumbe.”
Katika ujumbe huo ambao alikiri kuuandika, Mtatiro aliwataja wajumbe watatu ambao ni mawaziri kuwa waliwakaribisha wajumbe kwenye makazi yao na “kuwaandalia chakula cha kutosha, vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine, huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao hivyo vya siri.” Mmoja wa waliotajwa ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe aliyedaiwa kuwaalika wawakilishi wa wafugaji na kuwapa chakuka na bahasha.
Akijibu tuhuma hizo, pamoja na kukiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe na kula nao chakula, alikana tuhuma za kuwahonga ili waunge mkono msimamo wa chama hicho. Alisema Mtatiro amemdhalilisha, hivyo anawasiliana na mwanasheria wake ili kumfikisha mahakamani.

Chanzo: Mwananchi.

MAN CITY YAITWANGA SUNDERLAND NA KUCHUKUA CAPITAL ONE




‘Pandu Kificho ametusaliti’

Zanzibar. Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho amekiri kuwasilisha waraka kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba na kupendekeza Zanzibar na Tanganyika kuwa na mamlaka huru, hatua ambayo imezua malalamiko miongoni mwa makada wa chama hicho ambao wamesema huo ni usaliti.
Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma, Kificho ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), alisema kimsingi waraka huo ulilenga kuipa nguvu Zanzibar kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano ili kujiimarisha kiuchumi.
Kauli ya Kificho inakuja wakati baadhi ya wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar wakiitisha mkutano na kutoa tamko la kumshutumu kwa kutoa mapendekezo hayo, wakisema ni kinyume na msimamo wa chama hicho.
Kificho alionyesha kushangazwa na madai kuwa mapendekezo hayo yaliyoandaliwa na watu wanne ambayo ameyasaini si msimamo wa BLW.
“Tatizo lililopo ni tafsiri ya kila mmoja anapousoma waraka huo, hakuna sehemu tuliyoandika tunataka Serikali tatu, mamlaka huru maana yake kila upande uwe na uwezo wa kushughulikia mambo yake yasiyo ya Muungano na kujijenga kiuchumi, ikiwa ni pamoja Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) na siyo kuunda dola,” alifafanua Spika Kificho.
Alisisitiza kuwa angependa mambo ambayo hayamo katika orodha ya Muungano yaendeshwe na Zanzibar bila ya kuwekewa vikwazo mahali popote.
Madai hayo ni dalili za wazi za mgawanyiko baina ya wajumbe wa CCM ambao wameanza kuonyesha makundi mawili yenye misimamo tofauti.
Kundi linalomshutumu Kificho, linawajumuisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Juma Ali Shamhuna, Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha na Naibu Spika wa BWZ, Ali Abdallah Ali.
Jana, kundi hilo lilimtuhumu Kificho kuwa hakuwashirikisha wenzake katika mapendekezo Serikali tatu aliyoyawasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakisema  Baraza la Wawakilishi, kama taasisi, halikutoa msimamo wa pamoja.
Hata hivyo, mtazamo huo wa BLW unatofautiana na ule wa Kificho uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Othman Masoud Othman, ukipendekeza Serikali tatu.
“Kwa vile mfumo wa Serikali mbili uliopo sasa hauwezi kujenga Muungano utakaohimili mabadiliko ya kisiasa na kwa vile umejaribiwa na kuthibitishwa kuwa umeshindwa kujenga Muungano imara, uachwe katika kuendesha Muungano wa Tanzania,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ya Othman.
Jana asubuhi, zaidi ya wajumbe 10 wa Baraza la Wawakilishi akiwamo Shamhuna, Nahodha na Ali waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtupia lawama Kificho wakisema; “Amewasaliti katika mchakato huo wa Katiba.”

Sunday, March 2, 2014

Wanamgambo wa Nigeria wauwa watu 33

NIGERIA_5e951.jpg
Mabaki ya chuo cha serikali ambapo wanafunzi 60 walichomwa moto hadi kufa Februari 25, 2014
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa takribanu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali.
Mashahidi na maafisa wa ndani kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kundi linalotuhumiwa la wanamgambo wa Boko Haram limeuwa watu 33 na kushambulia kwa bomu chuo cha kidini katika jimbo la Adamawa.
Jeshi ambalo mara nyingi haliamini taarifa za idadi ya vifo kutoka kwa mashahidi limesema washambuliaji sita waliuwawa katika tukio hilo pamoja na mwanajeshi mmoja na raia watatu .
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa karibu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali karibu na jimbo hilo la Adamawa.
Chanzo, voaswahili. (R.M)

Chelsea yajiimarisha kileleni ligi kuu

CFC_910be.jpgTimu ya Chelsea imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuicharaza Fulham magoli 3-1 na kujikusanyia pointi 63.
Mabao yote matatu ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji wake Andre Schurrle akiyafunga katika dakika ya 52, 65 na 68, huku bao la kufutia machozi la Fulhamlikifungwa na Heitinga katika dakika ya 74.

Arsenal iliyokuwa ikifukuzana na Chelsea kwa tofauti ya pointi moja imejikuta ikiachwa pointi nne zaidi baada ya kucharazwa na Stoke goli 1-0. Arsenal imebaki na pointi 59 na kuporomoka hadi nafasi ya tatu, huku Liverpool ikipanda, nayo ikiwa na pointi 59 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga.
Wakati Newcastle ikiididimiza Hull kwa mabao 4-1, nayo Everton iliibanjuaWest Ham bao1-0.
Msimamo wa ligi kuu ya England baada ya michezo hiyo ya Jumamosi, Chelsea inaongoza kwa pointi 63 baada ya kucheza michezo 28 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 59 na Arsenal ni ya tatu ikiwa pia na pointi 59.
Mancity ni ya nne ikiwa na pointi 57 lakini ikiwa imecheza michezo 26 tu, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda kileleni iwapo itashinda mechi zake mbili.
Manchester United mabingwa watetezi, iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 45 lakini imecheza michezo 27.
Mkiani kabisa ni Fulham yenye pointi 21 na mbele yake ni Cardiff yenye pointi 22.
Chanzo, bbcswahili (R.M)

Obama aeleza wasi wasi wake kuhusu Ukraine







obama_edc89.jpg
Rais Barack Obama akizungumzia kuhusu hali nchini Ukraine.


Marekani imeonya kuwa rais Barack Obama pamoja na viongozi wengine wa Ulaya wataususia mkutano wa kundi la mataifa ya G8 mjini Sochi iwapo wataona kuwa Urusi inaingilia uhuru wa Ukraine.
Obama ameeleza wasi wasi wake mkubwa kuhusiana na ripoti kuwa majeshi ya Urusi yameingia mjini Crimea, kufuatia madai yaliyotolewa na afisa wa serikali mjini Kiev kuwa uvamizi umeanza.
Maafisa waandamizi wamesema rais ameamua kujitokeza katika ikulu ya Marekani ya White Housena kutoa maelezo baada ya nchi hiyo kuamua kuwa kulikuwa na ushahidi kwamba majeshi ya Urusi ni kweli yako ndani ya Ukraine.
Vikosi vyenye silaha nzito na katika sare ambazo hazina nembo ya taifa vimeonekana kuzunguka majengo ya serikali na katika uwanja wa ndege katika mji wa Crimea wa Simferopol , wakati maafisa wa Ukraine wakiishutumu Urusi kwa kile walichokiita uvamizi wa wazi.
Majeshi ya Urusi
Mzozo huo ulianzia katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi kufuatia kuondolewa kwa serikali inayoelemea upande wa Urusi mjini Kiev na kuingia katika mpambano wa kieneo baada ya madai ya maafisa wa Ukraine kuwa kiasi ya wanajeshi 2,000 wa Urusi wamewasili mjini Crimea.
"Tuna wasi wasi mkubwa sasa kuhusiana na ripoti za harakati za kijeshi zinazochukuliwa na shirikisho la Urusi ndani ya Ukraine," Obama amesema.
Afisa wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP baada ya taarifa ya rais kwamba " inaonekana kama wameingiza wanajeshi kadha nchini humo.
Afisa huyo amesema kuwa Urusi haijatoa tahadhari yoyote kabla kuhusu harakati hizo. Obama anatambua kuwa Urusi imekuwa na maslahi yake pamoja na uhusiano wa kiutamjaduni na kiuchumi na Ukraine, na imekuwa na maeneo ya kijeshi katika eneo la Crimea, eneo ambalo liliunganishwa na jamhuri ya zamani ya Kisoviet ya Ukraine katika umoja wa Kisoviet mwaka 1954.
Obama aonya
Lakini amesema ukiukaji wowote wa uhuru wa Ukraine pamoja na ardhi ya nchi hiyo utaiyumbisha kwa kiasi kikubwa Ukraine. "Marekani itasimama pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kusisitiza kuwa kutakuwa na gharama katika uvamizi wowote wa kijeshi nchini Ukraine," alisema rais Obama.
Afisa mwingine mwandamizi baadaye amedokeza kuwa gharama hizo zinaweza kujumuisha uamuzi wa Obama na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa Ulaya kususia mkutano wa nchi zenye utajiri mkubwa wa viwanda za G8 mkutano utakaofanyika katika mji wa kitalii uliofanyika michezo ya Olimpiki wa Sochi mwezi Juni.
Uwezekano mwingine wa kibiashara na kiuchumi ambao Urusi ilikuwa inataka hadi wiki hii huenda ukaingia katika hali shaka , afisa huyo amesema.
Urusi pia itavuruga nafasi yake ya kuonekana kuwa na mvuto duniani baada ya michezo ya majira ya baridi, ambayo ilimalizika mwishoni mwa juma lililopita, ameeleza afisa wa Marekani.
Chanzo, dw.de/swahili (R.M)

JK: HARAKISHENI SHERIA USALAMA MITANDAONI

 

Rais Jakaya Kikwete, akibofya kitufe kuzindua mtambo wa kuhakiki takwimu za mawasiliano kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dar es Salaam jana.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha mchakato wa Sheria ya Usalama kwenye mitandao unakamilika na kuanza kutumika, ili kudhibiti wanaotoa siri za nchi kwa kisingizio cha uhuru wa habari.
Hayo aliyasema jana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtambo maalumu wa usimamizi na uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS), iliyofanyika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dar es Salaam.

Rais Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo haitunzi siri zake, kwa kuwa jambo hilo ni muhimu kiusalama, hata kwa mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wa vyombo vya habari.
Alisisitiza kwa kumtolea mfano aliyekuwa Jasusi wa Marekani, Edward Snowden, anatuhumiwa kuvujisha siri za nchi hiyo kwenye mtandao, ambaye sasa amekimbilia mafichoni Urusi. Aliwapongeza TCRA kwa hatua hiyo, akieleza kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata kichocheo cha kukua kwa kuwa sasa kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano hasa ya simu za nje ya nchi na kuongeza kipato kwa taifa.
Awali Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema kufungwa kwa mitambo hiyo, kunakwenda pamoja na kuwapo kwa kanuni mpya za mawasiliano ya usimamizi na uhakiki wa mawasiliano ya simu (TTMS, Regulation 2013), ambapo imewezesha Serikali kupata senti 7 kati ya 25 zinazotozwa kwa kila dakika na nyingine zinagawanywa kwa kampuni husika.
"TCRA imefanikiwa kuilipa Hazina mgawo wa mwezi Oktoba, kwa mujibu wa Sheria ya TMMS Sh1.6 bilioni, leo tutakabidhi malipo ya Sh1.6 bilioni malipo ya Novemba hatimaye mwezi Machi tutalipa ya Desemba," alisema Nkoma.
Chanzo, mwananchi (R.M)