Tuesday, March 4, 2014

Serikali ya Burundi yakanusha tuhuma za kuhujumu vyama vya upinzani

Willy Nyamitwe, naibu msemaji wa rais wa Burundi akiwa katika studio za RFI jijini Paris

Serikali ya Burundi imekanusha tuhuma za kuingilia shughuli za vyama vya upinzani kwa lengo la kuvidhoofisha kama inavyodaiwa na vyama hivyo. Charles Nditije anaye kubalika kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Uprona, amesema kuwa chama tawala kinahusika katika matukio mengi ya kuvigawa vyama vya kisiasa, kwa malengo ya kujizatiti katika uchaguzi ujao. Mwishoni mwa mwezi Januari, Waziri wa Mambo ya Ndani Edouard Nduwimana alibadili maamuzi na kutangaza kumtabuwa Bonaventure Niyoyankana ambaye aliondolewa kwenye uongozi kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Uprona Badala ya Charles Nditije. Hatuwa ambayo ililaaniwa vikali na wafuasi wa chama Uprona.

Hata hivyo aliyekuwa makam wa kwanza wa rais kutoka chama Uprona alifuta maamuzi hayo ya waziri wa mambo ya ndani na hatimaye kufutwa kazi na rais wa jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza, hatuwa ambayo ilichukuliwa kama hujuma dhidi ya chama hicho na njama za kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Utata uliopo ni mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo ambapo vyama vya upinzani vinakituhumu chama tawala cha Cndd-Fdd kuwa na dhamira ya kufanya mabadiliko ya katiba, ili kumpa nafasi rais wa sasa kuwania muhula mwingine watatu.
Hata hivyo chama tawala nchini burundi hakijabainisha nani ataye wania urais mwaka 2015, licha ya kuendelea kutetea kuwa rais Nkurunziza bado ananafasi ya kuwania urais, kwani alichaguliwa na wananchi kwa muhula mmoja na umebaki muhula mwingine wa kuchaguliwa na wananchi.
Wanasiasa nchini Burundi wamekuwa wakiweka wazi kuhusu katiba ya Burundi iliofikiwa jijini Arusha nchini Tanzania, inayo baini kuhusu uongozi, na ugavi wa madaraka kati ya watu wa makabila ya wahutu na watutsi.
Tayari Chama cha Uprona kinachatajwa kuwa na wafuasi wengi wa kabila la watutsi, kimesema inavyoelekea kwa sasa chama tawala kinataka kuvunja mkataba wa Arusha na kuwanyima nafasi Watutsi jambo ambali msemaji wa chama Uprona tawi la Charles Nditije, Bonaventure Gasutwa anasema ni hatari sana.
Akihojiwa jana jijini Paris na Idhaa ya Kifaransa ya RFI naibu msemaji wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe, amesema walichokifanya ni kurejesha taasisi tawala baada ya baadhi ya wafuasi wa chama Uprona kujiondowa, na wapo sahihi kwakuwa walifuata sheria.
Kuhusu swala la usawa wa kikabila katika taasisi za uongozi, Willy Nyamitwe amesema katika chama tawala cha Cndd-fdd kuna watutsi wengi kuzidi idadi ya waliomo katika chama Uprona, hivyo usawa bado waendelea kutekelezwa
Aidha kuhusu mjadala uliopo juu ya rais wa sasa kuwania urais au la, Naibu msemaji wa rais Nkurunziza amesema baadhi wanaonakuwa rais Nkurunzia anaongoza muhula wa pili na wengine wanaonakuwa ni muhula wake wa kwanza ambapo alichaguliwa moja kwa moja na wananchi, na hapa ndipo mjadala unazunguukia, lakini ameendelea kusema huu mjadala haustahili kuwepo kwakuwa chama cha Cndd-fdd hakijafanya kongamano na kuamuwa nani atasimama kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment