Tuesday, March 4, 2014

Kesi ya mauaji ya bingwa wa mbio za paralympic Oscar Pistorus inaendelea

Оскар Писториус в зале суда в Претории 03/03/2014

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mwenye ulemavu wa Miguu Oscar Pistorius raia wa Afrika Kusini, hii leo imeingia siku yake ya pili kwa upande wa utetezi kuwahoji mashahidi wa Serikali.

Hii leo shahidi wa pili kwenye kesi hiyo ambaye ni jirani wa Oscar Pistorius ameieleza mahakama namna alivyosikia milio ya risasi na kelele za kuomba msaada toka kwa mpenzi wa Pistorius na kwamba jambo hilo lilimfanya ahisi kulikuwa na ujambazi kwa jirani yake.
Lakini wakati shahidi huyu wapili akieleza kile alichokisikia, hapo jana shahidi wa kwanza kwenye kesi hiyo alijikuta matatani wakati akihojiwa na upande wa utetezi kutokana na kutofautiana kwa kauli zake na hata wakati fulani kuangua kilio kilichopuuzwa na mawakili wa Pistorius.
Katika hatua nyingine jaji anayesikiliza kesi hiyo, Thokozile Masipa amevionya vyombo vya habari dhidi ya kuchapisha picha za mashahidi ambao wamekataa sura zao kuoneshwa hadharani na kwamba atavichukulia hatua vyomb vyote vya habari vitakavyokiuka amri ya mahakama.
Hapo jana kituo kimoja cha televisheni nchini humo kilionesha picha ya shahidi ambaye ni mhadhiri wa chuo kimoja mjini Pretoria wakati akihojiwa na upande wa utetezi hali iliyoamsha toka kwa wanaharakati.

No comments:

Post a Comment