Tuesday, March 4, 2014

Urusi yaionya Marekani dhidi ya vitisho

mkutano wa vyombo vya habari wa rais wa Urusi Vladimir Poutine, March 4, 2014 jijini Moscou

Nchi ya Urusi imeionya serikali ya Marekani dhidi ya hatua yoyote iliyopanga kuchukua ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuongeza kuwa atakaeumia kwenye mzozo huo atakuwa ni Marekani mwenyewe. Kauli ya Urusi inatolewa wakati huu ambapo rais wa Marekani Barack Obama akitishia kusitisha ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Urusi ambapo pia amesharangaza kusitisha ushirikiano wa kijeshi na taifa hilo kufuatia hatua yake ya kuivamia nchi ya Ukraine. Urusi inasisitiza kuwa inauwezo wa kusimama yenyewe hata bila ya kutegemea wafanyabiashara toka nchini Marekani.



TWaziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amewasili nchini Ukraine jumanne hii ambapo atakuwa na mazungumzo na utawala wa mpito wa taifa hilo ambao wameomba msaada toka jumuiya ya kimataifa.
Ziara ya Kerry inafuatia ziara kama hiyo ambayo imefanywa hapo jana na waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague ambao wote kwa pamoja wanalenga kusisitiza kutoridhishwa kwao na namna ambavyo Urusi imeivamia kijeshi nchi ya Ukraine.
Tayari waziri mkuu mpya wa Ukraine, Arseni Iatsenuik ametoa matamshi mengine kukashifu utawala wa Urusi na kuionya kuhusu kuendelea kusonga mbele kwa vikosi vyake kwenye mji wa Crimea.
Kauli ya Arseni iliungwa mkono na waziri mkuu wa Uingereza David cameron ambaye amesisitiza kuwa nchi yake itachukua hatua kali dhidi ya Urusi iwapo itaendelea kuingilia uhuru wa taifa hilo.
Awali wakati wa kikao cha tatu cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Urusi Vitaly Churkin alitetea uamuzi wa nchi yake kupeleka wanajeshi kwa kile alichodai waliombwa kufanya hivyo na rais aliyeoondolewa madarakni Viktor Yanukovich.
Kauli ya Churkin inakosolewa vikali na balozi wa Marekani kwenye umoja huo, Samantha Power ambaye amekiita kitendo cha urusi kama ni chakutaka kuhalalisha jambo haramu.

Katika hatua nyingine rais Vladmir Putin kwa mara ya kwanza amezungumza na wanahabari na kusisitiza kuwa wanajeshi wake hawakushiriki oporesheni zozote za kuteka bunge la Crimea wala kuwaweka mateka wanajeshi wa Ukraine.

No comments:

Post a Comment