Mshambuliaji Manchester United Robin van Persie amesema rasmi kwamba anataka kubakia Old Trafford kwa muda mrefu.
Mwanasoka
huyo mwenye umri wa miaka 30 amekanusha kwamba haelewani na kocha David
Moyes na imekuwa ikisemekana kwamba angeondoka kwenye timu hiyo kipindi
kijacho cha usajili.
Lakini nahodha wa Uholanzi anasisitiza kwamba anapendelea kubakia United.
"Ukweli
ni kwamba nina furaha sana," Alisema. "Nilisaini mkataba wa miaka minne
na nina furaha kuendelea kukaa hapa kwa muda mrefu, hata baada ya miaka
yangu miwili iliyobaki."
Pia tetesi zimekuwa zikisema kwamba Van Persie havutiwi na mbinu za ufundishaji za Moyes.
Lakini
akiongea katika interview aliyofanyiwa na United Review, kuelekea
mchezo dhidi ya mahasimu wao Liverpool, aliongelea juu ya saula la mbinu
za Moyes.
"Hakuna
shaka kwamba ninajifunza mbinu mpya na ninaendelea vizuri chini ya
David Moyes," alisema. "Vipindi vya mazoezi tunavyokuwa kuwa navyo ni
vizuri mno na ninajifunza vitu vingi kutoka kwenye mazoezi hayo kila
siku.
"Kuna
hali nzuri ya kuheshimiana baina yetu na mazingira yetu ya kufanya kazi
ni mazuri. Moyes anataka sana kazi iende vizuri na mie ninataka hivyo
pia."
No comments:
Post a Comment