Wednesday, October 31, 2012

KIMBUNGA CHA SANDY CHASABABISHA HASARA ZAIDI YA DOLA BILIONI ISHIRINI.




MAREKANI,
Rais wa Marekani Barack Obama atangaza majimbo ya kaskazini mashariki ya Marekani ya New York na New Jersy kuwa maeneo ya "maafa makubwa" baaada ya kimbunga kikubwa kilichopewa jina la Sandy.

Tangazo hilo limetolewa hapo jana siku ya jumanne na linaruhusu kutumika kwa fedha ya serikali katika maafa hayo.

Kimbunga Sandy kilifika nchi kavu siku ya Jumatatu jioni na kinaendelea kupunguka nguvu zake kinapita sehemu za kati na kaskazini ya marekani. Maafisa wanasema watu 16 walifariki katika katika maeneo ya mashariki ya Marekani kutokana na kimbunga hicho ambacho kilisababisha vifo vya watu 65 wiki iliyopita katika nchi za Caribbean.

Kwa siku ya pili mfululizo shughuli zote za serikali na biashara pamoja na shule katika miji mikubwa mashariki ya Marekani ziliendelea kufungwa siku ya Jumanne wakati mamilioni ya watu wakiwa hawana huduma ya umeme.

Takriban wasafiri elfu 10 walikwama katika miji hiyo ya mashariki ya nchi baada ya maelfu ya safari za ndege kuahirishwa kwa siku ya pili. Halikadhalika huduma za usafiri wa mijini iliendelea kufungwa na mjini New York kumekuwepo na mafuriko ya maji katika njia za reli za chini kwa chini.

Watalamu wa uchumi wanatabiri kwamba kimbunga Sandy huwenda kimesababisha hasara inayogharimu takriban dola bilioni 20.(VOA)

CHELSEA YAMTUHUMU MWAMUZI DHIDI YA MATAMSHI YA KIBAGUZI KWA MIKEL OBBI




LONDON-UINGEREZA,
Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imemtuhumu mwamuzi aliyechezesha wa mchezo wao na Manchester United Mark Clattenburg kumtolea maneno ya kibaguzi kuungo wake raia wa Nigeria John Mikel Obi. Msemaji wa Chelsea ameweka bayana wameshawasilisha malalamiko yao ili hatua zichukuliwe dhidi ya Clattenburg ambaye amekumbana na ukosoaji mkubwa kwa kile kinachoelezwa ni kushindwa kuumudu mchezo huo. Chama cha Waamuzi wa Kulipwa PGMO kimekiri kupokea malalamiko hayo na kusema watayafanyia kazi kwa kadri ambavyo itaonekana na uchunguzi utafanyika ili kubaini iwapo Clatternburg alitoa maneno ya kibaguzi kwa Mikel Obi. Katika mchezo huo Manchester United ilivunja mwiko wa kushindwa kupata ushindi kwenye michezo ya Ligi Kuu katika uwanja wa Stamford Bridge kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-2. Chelsea ililazimika kumaliza ikiwa na wachezaji tisa baada ya kushuhudia Branislav Ivanovic na Fernando Torres wakilimwa kadi nyekundu kitu ambacho kilizusha lawama za kila mara kwa mwamuzi Clattenburg. Manchester United ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa David Luiz ambaye wakati anaokoa akaukwamisha mpira wavuni kabla ya Robin Van Persie kufunga goli la pili na kushuhudia Juan Mata akifunga goli la Chelsea kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili Chelsea waliongeza kasi na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Ramires kabla ya Javier Hernandez hajafunga goli la tatu na la ushindi dakika kumi na tano kabla ya mchezo kumalizika na kuiba ushindi Manchester. Goli la Hernandez lilizidisha hasira kwa wachezaji wa Chelsea na hata mashambiki wake kutokana na kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea na halikustahili kuwa goli na kushuhudia Mikel Obi akilimwa kadi ya njano kwenye malumbano hayo. Kwa matokeo hayo sasa Chelsea inaendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi moja baina yake na Manchester United ambayo imepiteza michezo mieili tangu kuanza kwa Ligi msimu huu na huu ukiwa mchezo wa kwanza kwa The Blues kufungwa.(Chanzo RFI)



Friday, October 26, 2012

OBAMA APIGA KURA ZA AWALI-AVUNJA REKODI.


CHICAGO-MAREKANI, Rais Barack Obama wa Marekani amepiga kura ya awali hapo jana na kuwa rais wa kwanza kupiga kura ya awali. Obama amepiga kura hiyo katika mji wa Chicago ambako ndiyo nyumbani kwao. Obama yupo katika kampeni ya siku mbili katika majimbo nane yanayotegemewa kutoa mshindi wa Urais kutokana na kutokuwa na ushabiki wa Chama likiwepo jimbo kubwa la Ohio.
Upigaji kura huo wa rais Obama umekuwa sehemu ya kampeni za Rais huyo ambaye amewahamasisha watu kupiga kura mapema, ambapo mpaka sasa inakasdiriwa watu zaidi ya milioni 7 wameshaoiga kura zao na hivyo kufanya vituo zaidi ya asilimia 35% kuwa tayari vimepigiwa kura siku ya uchaguzi.
Mfumo huo wa kupiga kura mapema ni muhimu kwa watu ambao huwa na udhuru au kuhofia kutokuwepo siku ya kupiga kura.
Wakati huo huo wanakampeni wa Rais Obama wameunga mkono ndoa za Kishoga katika majombo matatu ya Washington,Maryland na Maine ambako kura za maoni zinapigwa kuhusu kurudisha au kuondoa ndoa hizo.
Mpinzani wake Mitty Romney alikuwa Ohio hapo jana katika kampeni huku kura za maoni zikionesha Mitty Romney akiongoza kwa asilimia kadhaa zikiwemo asili mia 54 kwa 49 kwa 47 katika kituo cha habari cha BBC ya Uingereza na asilimia 52 ya watu wakipiga kura za umwamini Mitty Romney katika uchumi dhidi ya asilimia 47 wanaomwamini Obama katika katika kituo cha habari cha ABC.



Thursday, October 25, 2012

ISRAEL NA PALESTINA WASHAMBULIANA KIJESHI



ISRAEL/PALESTINA,  Majeshi ya Palestina yamerusha maroketi zaidi ya 40 kuelekea Israel hapo jana huku isarel na wenyewe wakifanya mashambulizi ya anga kuelekea Ukanda wa Gaza.



Kwa mujibu wa hospitali huko Gaza  zimesema kuwa Wanajeshi watatu waliokuwa wakijiandaa kufanya Shambulio la Roketi waliuawa  Wna wenginei wengine wanane kujeruhiwa, huku shambulio kuelekea Israel likijeruhi watu kadhaa.

Mashambulio hayo yamefuatia  mwanajeshi mmoja wa Israeli kujeruhiwa vibaya katika Shambulio la Bomu alipokuwa akifanya Doria mpakani  Kissufin eneo la Gaza hapo juzi.

Chama cha Hamas kimethibitishwa waliouawa kuwa wanajeshi wake huku waziri Mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu akiahidi kulipa kisasi kwa Gaza amabao amewatuhumu kuungwa mkono na Tehran.

Monday, October 22, 2012

Wapiganaji wa kigeni waingia Mali Kaskazini

Mamia ya wanajihadi kutoka nje ya nchi ya Mali wameripotiwa kuwasili kaskazini mwa nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kupigana na wanamgambo wa kiislamu wanaomiliki eneo la kaskazini mwa Mali wakati vikosi vya kimataifa vikitarajiwa kuingilia kati mzozo wa Mali. Wakazi wa Mji wa Timbuktu, Gao na Maafisa usalama wa nchini Mali na Makamanda wa makundi ya kiislam wamethibitisha kuwa kumekuwa na wimbi la wapiganaji wa kigeni wanaoingia kaskazini mwa Mali kwa zaidi ya siku mbili zilizopita. Kuwasili kwa wanajihadi hao kutoka Sudan na Sahara Magharibi, kunatokea siku mbili tu baada ya mkutano wa kimataifa wa nchi washirika wa Mali ambao umedhamiria kuongeza mshikamano na serikali ya Mali kurudisha eneo hilo. Wakati huohuo,Serikali ya Ufaransa inatangaza kurejelea ushirikiano wake wa kijeshi na nchi ya Mali, Ushirikiano ambao ulisimamishwa tangu jaribio la mapinduzi ya tarehe 22 ya mwezi Machi 22 mwaka Wimbi hilo la wapiganaji limeingia wakati huu ambapo jumuia ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika,ECOWAS ikiendelea na harakati za kuvamia kaskazini mwa nchi hiyo na kusambaratisha Makundi ya kiislamu katika eneo hilo.(Chanzo RFI)

MWAKYEMBE AKABIDHIWA RIPOTI YA BANDARI

DAR ES SALAAM-TANZANIA, WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), huku akitoa onyo kali kwa vigogo waliokwepa kuhojiwa na kamati kwa visingizio mbalimbali akisema ni lazima watahojiwa tu. Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo yenye kurasa 285 na Mwenyekiti, Wakili Benard Mbakileki, na kuongeza kuwa kama suala analotaka kuhojiwa mhusika linahusu polisi, atapelekwa mbele ya jeshi hilo. Waziri Mwakyembe alitoa kauli hiyo baada ya Wakili Mbakileki kueleza kuwa baadhi ya watu muhimu TPA waliotakiwa kuhojiwa walikwepa kwa visingizio mbalimbali ikiwamo kuuguliwa, kufiwa na wengine kuzima simu kabisa. Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema: “Kama walidhani kukwepa kamati ndio mambo yameisha, wanajidanganya. Watakuja kujibu mbele yangu na kama mambo yanahusu polisi tutawapeleka, hatutaacha mtu.” Aliongeza kuwa kamati hiyo imefanya kazi ya kizalendo na kuahidi mambo yote iliyopendekeza watayafanyia kazi hatua kwa hatua, ili kuboresha bandari hiyo. “Niwahakikishie hii kazi mliyoifanya haitakwenda bure, hadi kufikia Desemba mwaka huu, tutakuwa tumeyafanyia kazi mambo yote mliyopendekeza. Tutataka kuipa bandari sura mpya, kwa sasa inakosa ufanisi…tutakuja na uamuzi ambao hakitadokolewa kitu, kwani watakaodokoa, nao watadokolewa, kwani tusipofanya uamuzi huo hatutaikomboa nchi yetu,” alisema. “Tulikuwa tunasikia habari za Twiga kusafirishwa kwenye ndege watu wakashangaa, lakini pale bandarini kontena na ukubwa wake linayeyuka. Mwaka juzi yaliyeyuka makontena 10, mwaka jana 26 na mwaka huu mawili na mambo yanatufanya tusiaminike,” alisema. Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo, watafanya kazi kwa gharama yoyote, bila kumwonea mtu, ili kurekebisha bandari hiyo aliyoeleza kuwa iwapo ingesimamiwa vizuri nchi ingeweza kuendesha mambo mengi. Aidha, alibainisha kuwa tangu kamati hiyo ilipoanza kufanya kazi, baadhi ya nchi jirani zimeanza kurejesha imani na bandari hiyo zilikemo Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Rwanda na Burundi. Aliongeza kuwa iwapo baadhi ya watu wanakerwa na mabadiliko ndani ya TPA, waondoke kwani mjini kuna kazi nyingi za kufanya. Pamoja na mambo mengine, Mwakyembe aliomba wapatiwe muda wa kuipitia ripoti hiyo kwa umakini na kwamba kila hatua watakuwa wakitoa taarifa kwa umma.(Chanzo:Bongonewztz)

FIDEL CASTRO AONEKANA TENA



HAVANNA-CUBA,
Kiongozi mwanamapinduzi wa Bw. Fidel Castro(86) ameonekana kuwa katika hali nzuri tofauti na uvumi baada ya kukutana na aliyewahi kuwa makamu wa rais wa Venezuela Bw. Elias Jaua hapo jumamosi iliyopita.Jaua ambaye ameonesha picha za kiongozi huyo na kuwaambia waandishi wa habari kuwa kiongozi huyo yupo katika hali nzuri.

Fidel Castro hajaonekana hadharani tangu mwezi Machi mwaka huu alipokutana na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa Benedict XVI.Tangu wakati huo kiongozi huyo hajaonekana hadharani na kuzua utata juu ya afya yake huku wengi wakivumisha yupo mahututi na wengine wakidai amefariki.

Tangu kuonekana kwake mwezi Machi kiongozi huyo amekuwa akitoa hotuba zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari bila ya yeye kutokea huku baadhi ya hotuba hizo kuonekana zina dosari kiasi na kuzua maswali kuhusu afya ya kiakili ya kiongozi huyo.

Bw.Jaua ambaye anagombea ugavana katika jimbo la Miranda huko venezuela amesema waliongea na Fidel Castro katika Hoteli ya Havana na waliongea kuhusu mambo mengi yakiwemo kilimo na siasa,"Ndiyo nimeonge na Fidel jana alikuwa vile vile kama yule Fidel wa zamani na mashavu yake ya pink," Martinez aliliambia shirika la Reuters.


Friday, October 19, 2012

WINGU LA VURUGU ZA KIDINI LAENDELEA KUTANDA TANZANIA

TANZANIA,
Vurugu zinazohusishwa na dini zimeendelea nchini zikisababisha  kuuawa kwa askari polisi mmoja kisiwani Zanzibar, maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoa tamko zito, pamoja nakupandishwa kizimbani kwa Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda (54) na wenzake 49 pamoja na tukio la Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kususia kikao. 

Askari aliyeuawa ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia huko Zanzibar Koplo Said Abdulrahman, ambaye ameuawa kwa kupigwa mapanga na wafuasi wanaodaiwa ni wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (Jumiki) katika vurugu zinazoendelea mjini Zanzibar baada ya kiongozi wa kikundi cha uamsho sheikh Farid kupotea na kuibuka hisia za kushikiliwa na jeshi la polisi kwa siri.

kwa mujibu wa Jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema wafuasi wa Uamsho walimvamia askari huyo majira ya saa 6:30 siku ya jumatano eneo la Bububu ambapo walimshambulia na kuichoma piki piki aliyokuwa anaitumia


kwa mujibu wa jeshi lapolisi kisiwani humo watu 10 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho pamoja na vurugu.


Wakati huohuo,kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar lilivamiwa na wafuasi wanaoaminika kuwa ni wa kundi la Uamsho na kusababisha uharibifu wa mali ikiwamo kuvunjwa vioo na madirisha kung’olewa.

kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Masoud, alisema wafuasi wa Uamsho walilivamia kanisa hilo na kulishambulia kwa mawe.

APPLE WASHINDWA RUFAA YA KESI DHIDI YA SAMSUNG

LONDON-UINGEREZA,
http://www.digitaltrends.com/wp-content/uploads/2012/09/iPhone-5-vs-Galaxy-S3-angle-left-side-by-side.jpgMahakama ya rufaa nchini Uingereza imeipa ushindi kampuni ya Samsung ya Korea dhidi ya mahasimu wao kampuni ya Apple ya nchini Marekani.Katika kesi hiyo ambayo Apple wanailalamikia Samsung kwa kutengeneza simu za Samsung Galaxy zenye muundo unaofanana na wa simu zao za Iphone walikuwa wakitaka kusimamishwa kwa uuzwaji wa simu hizo barani Ulaya.

Katika maamuzi hayo mahakama imekiri kuwa simu za Samsung zinafanana na zile za Apple lakini ikaongeza kuwa hazina uhusiano na uigaji wa aina yoyote kutoka kwa simu za Apple, pamoja na maamuzi hayo mahakama imeitaka kampuni ya Apple kutangaza katika tovuti yake na baadhi ya magazeti yatakayoamriwa kuwa Samsung hawakunakili muundo wao.

Kampuni ya Apple imekataa kuongelea chochote juu ya suala hilo huku Samsung wakisema wamepokea kwa furaha uamuzi huo.

Monday, October 15, 2012

MKUTANO WA FRANCOPHONE WAFUNGWA.

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/4f48dfca7accc969fc3ad0912c4afc14_L.jpgMkutano wa wakuu wa umoja wa nchi zinazotumia lugha ya kifaransa Francophone ulifungwa jana huko Kinshasa, baada ya kupitisha maazimio kuhusu Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Mali.
 Katika mkutano huo viongozi hao wwamekubaliana kuheshimu umoja na ukamilifu wa ardhi wa Mali na kutaka kuimarisha mchakato wa mazungumzo kati ya pande zote nchini Mali, ili kuleta utulivu wa hali ya kisiasa nchini humo.

Kuhusu mgogoro wa Demokrasia na Rwanda viongozi hao wamezitaka nchi hizo ziendelee na mazungumzo ya kuimarisha uaminifu baina yao ili kuondoa mgogoro unaozikabili kuhusu mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Viongozi hao pia waliitaka jumuiya ya kimataifa kuwa na mkutano wa kujadili kuimarisha mapambano dhidi ya uharamia katika Ghuba ya Guinea.

Mkutano huo uliwakutanisha wakuu 15 wa serikali za nchi zinazozungumza kifaransa, mkutano ujao umepangwa kufanyika Senegal mwaka kesho

Saturday, October 13, 2012

UMOJA WA KIMATAIFA WAANDAA MPANGO WA KUISHAMBULIA MALI KIJESHI



BAMAKO-MALI,
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limethibitisha mpango wa kushambulia waasi walioivamia sehemu ya nchi ya Mali huku likitoa siku 45 kwa nchi za Afrika magharibi kutoa taarifa kuhusu mpango wa makubaliano uliopo.

 Ujumbe huo uliothibitishwa na baraza hilo Ijumaa ya jana umeutaka utawala wa Bamako na wawakilishi wa waasi wa Tuareg pamoja na waoiganaji wa kiislamu wanaotawala kaskazini kujihusishakatika mapatano.
Wanachama hao wameonya kuwa mpango huo uzingatie mtazamo wa kuleta umoja,uimara na uhuru wa kisiasa nchini Mali.

Mali imegawanyika tangu mwezi machi mwaka huu baada ya rais wa nchi hiyo kupinduliwa hali iliyowafanya waasi wa Tuareg kuteka sehemu kubwa ya nchi hiyo wakishirikiana na waasi wa kiislamu wenye uhusiano na Al-Qaeda.