Sunday, February 12, 2012

CHELSEA HOI KWA EVERTON- yafungwa 2-0, Pienaar awa mwiba.


Mchezaji wa afrika Kusini Steven Pienaar alikuwa mwiba mkali Everton ilipoichapa Chelsea Kwa magoli 2-0, akifunga goli la kwanza huku lile a pili likifungwa na Muagentina denis Stracqualursi katika kipindi cha pili.
Evertonambao hapo jana walikuwa wenyeji katika uwanja wao wa Goodison Park walianza kwa kasi na kufanikiwa kuapata goli lao la kwanza katika dakika ya 5 baada ya mpira uliomgonga Frank lampard Kumkuta Pienaar ambaye alipiga shuti kali la karibu lililomshinda kipa Petr Cech.

Everton nusura wapate goli la pili katika dakika ya 18 wakati Petr Cech aliposhindwa kuondoa mpira katika hatari na kumkuta Landon Donovan nje kidogo ya kumi na nane amabapo hata hivyo shuti lake hafifu liliokolewa na kipa huyo.
Chelsea nao walijitahidi kuongeza nguvu katikati mwa kipindi cha kwanza ambapo walikaribia kupata goli katika nafasi mbili ya kwanza katika dakika ya 25 ambapo shuti la michael Essien liliokolewa na Mlinzi wa Everton na lile lililofuatia la daniel Sturridge liliokolewa pia, huku nafasi nyingine ya Juan Mata ambaye alipiga shuti baada ya kupokea mpira kutoka kwa Sturridge ndani ya Eneo la penati liliishia kumgonga mlinzi wa Everton na kuwa Kona.

Hata hivyo chelsea walishindwa kuendeleza mikiki mikiki hiyo katika kipindi cha pili na kujikuta wakifungwa goli la pili dakika ya 72 katika kipindi cha pili baada ya Neville kumnyang'anya mpira Ashley Cole na Kumkuta Laandon Donovan ambaye alipiga shuti kali lililompita Petr cech licha ya kulipangua na kutua wavuni.

Licha ya kupigana zaidi Chelsea walishindwa kubadilisha matokeo na hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa 2-0,na kuwafanya wenyeji hao wa Stamford bridge wakishindwa kuondoka na Point tatu katika mechi nne mfululizo.

No comments:

Post a Comment