Saturday, February 4, 2012

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA- GUINEA NA SUDAN ZATUPWA NJE ZAMBIA NA IVORY COAST ZAPETA.




MALABO-GUINEA, Ivory coast imezima ndoto za moja ya wenyeji wa kombe la mataifa ya afrika mwaka 2012 Guinea bissau kusonga mbele katika nusu fainali baada ya Kuirarua kwa jumla ya mabao 3-0, magoli yakifungwa na Didier Drogba Katika dakika ya 36 na 69, pamoja na Yaya Toure dakika ya 81.

Ivory coast walistahili kushinda mechi hiyo hasa kutokana na kuonesha kiwango kizuri na kutawala mchezo tangu mwanzo hata hivyo wanapaswa kujilaumu kwa kukosa nafasi nyingi za wazi ikiwemo Penati iliyopigwa na Didier dgorgba na kuokolewa na kipa wa Guinea katika Dakika ya 29 na pamoja ile ya wilfred Borni dakika ya 93 alipopiga shuti lililopita sentimeta chache pembeni ya goli baada ya kubaki na kipa.

Kwa matokeo hayo wenyeji hao wameyaaga mashindano hayo na Ivory coast itamsubiri mshindi kati ya Gabon na mali katika robo fainali nyingine hapo jumapili.



katika robo fainali ya kwanza Zambia nao walikata tiketi ya Nusu fainali baada ya kuwafunga Sudan kwa jumla ya magoli 3-0, magoli ya zambia yakifungwa na
Stoppila Sunzu dk 15, Chrios Katongo dk 66 na James Chamanga dk 86. Kwa matokeo hayo Zambia itamsubiri mshindi kati ya Tunisia na Ghana hapo kesho.



No comments:

Post a Comment