Sunday, February 12, 2012

ARSENAL WAIBURUZA SUNDERLAND-


Thiery Henry ameipatia ushindi mwingine Arsenal hapo jana ilipocheza na Sunderland, na kuifanya timu kushinda kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya kutanguliwa kwa goli moja na Sunderland katika uwanja wa Light.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilishuhudia Arsenal ikifanya mashambulizi machache kutokana na ulinzi imara wa Sunderland ingawa Arsenal walionekana kutawala kiasi kipindi hicho wakitumia nguvu za ziada kuwapita viungo na mabeki wa Sunderland.

Kipindi cha Pili kilianza kwa Arsenal kufanya mashambulizi ingawa bado awakufua dafu kwa safu ya ulinzi ya sunderland. Badala yake Sunderland ndio walioanza kufanya mashaambulizi kupitia kwa Craig Gardner katika dakika za 61na 63 na kumfanya kipa wa Arsenal Wojciech kufanya kazi ya ziada.
hatiimaye Sunderland walipata goli lao dakika ya 70 baada ya makosa ya mlinzi wa Arsenal ambaye alipoteza mpira na kumfanya james Mc Clean kufunga goli hilo.

Baada ya goli hilo Arsenal nao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 75 kupitia kwa machezaji Aaron Ramsey aliyepiga shuti lililogonga mwamba na kuingia golini.

Na mwishowe matokeo yakiwa yanaonekana kuwa sare Mchezaji anayeshika vichwa vya habari tangu arudi tena kwa muda Arsenal mkongwe thiery Henry alifunga Goli katika dakika ya 91 ya ambao ulikuwa ni muda wa nyongeza akiunganisha krosi ya Andrei Arshavin na kuifanya Arsenal kuibuka na Ushindi wa magoli 2-1.

Thiery Henry ambaye amerudi Arsenal kwa muda kutoka Marekani ambako anacheza soka kwa sasa amekuwa chachu na msaada wa ushindi wa Arsenal katika siku za hivi karibuni na pengine timu hiyo inauwezekano wa kufikiaria kumrudisha katika kikosi hicho cha Arsene wenger.

No comments:

Post a Comment