Thursday, February 9, 2012

MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA WAFIKIA KIKOMO-Katibu mkuu na mganga mkuu wasimamishwa kazi.

DAR ES SALAAM-TANZANIA,
Mgomo wa Madaktari wa hospitali za umma nchini tanzania hatimaye umefikia kikomo leo hii huku kukishuhudiwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya ndugu. Blandina Nyoni na mganga Mkuu wa wa serikali bw. Deo Mtasiwa wakisimamishwa kazi kupisha Uchunguzi dhidi yao.

Hatua hiyo imekuja wakati waziri mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Pinda alipokutana na madaktari hao pamoja na wawakilishi wa wale wa mikoani kujadili suala hilo.
Katika kikao hicho serikali imekubali kuyashugulikia madai ya madaktari hao ambayo ni pamoja na Nyongeza ya mishahara, mazingira mazuri ya kazi na Marupurupu mengine ambay madaktari hao wanaidai Serikali.

Kwa Makubaliano hayo serikali na madaktari hao wamekubaliana kusitisha mgomo huo na Kurudi kazini kuanzia hapo kesho siku ya Ijumaa.
Mgomo huo umedumu kwa muda wa wiki tatu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa kawaida ambao serikali za umma ndio kimbilio lao.

No comments:

Post a Comment