Thursday, February 9, 2012

IVORY COAST YAIFUATA ZAMBIA FAINALI, YAWATOA MALI.



Goli la nguvu na juhudi binafsi lake Mchezaji mahiri wa Ivory Coast anayeichezea Arsenal ya uingereza Yao Gervinho jana lilikuwa tosha kuwaingiza tembo kutoka magharibi ya Afrika katika fainali.
Gervinho ambaye tangu mwanzo wa mashindano haya kuanza alionekana kuwa katika chini ya kiwango jana aligeuka mwabi makali kwa goli lake hilo mahiri kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Ivory coast ambao walionekana kuwa moto tangu mwanzo wa mchezo kwa kuwakosa mali katika dakika ya 6 ya mchezo baada ya kichwa cha Didier Drogba kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Dakika kumi baadae baada ya shambulizi hili Salomon kalou alitoa pasi murua iliyomkuta Yaya Toure katika nafasi nzuri ya kufunga ingawa safu ya ulinzi ya Mali iliokoa shambulizi hilo.

Mwishowe katika dakika ya 45 Gervinho aliiandikia Goli timu yake baada ya juhudi binafsi ambapo alitumia kasi aliyonayo kusonga mpaka golini kutoka kati kati ya uwanja akitumia upande wa Kushoto na baadae kurudi kulia akiwa ndani ya eneo la kumi na nane na kufunga kwa mguu wa kulia.

katika kipindi cha pili hakukuwa na ushindani mkali kama kile cha kwanza ingawa timu zote mbili zilitengeneza nafasi ya kufunga, lakini bahati mbaya kwa Mali ambao hawakuweza kurudisha goli hilo mpaka mwisho wa mchezo.

Kwa matokea hayo mali watacheza na zambia siku ya Jumamosi kumtafuta mshindi wa 3, huku Ivory coast wakiwafuata Zambia katika fainali zitakazochezwa hapo jumapili ya tarehe 12 wezi huu Katika mji wa libreville.


No comments:

Post a Comment