Saturday, February 11, 2012

IRAN KUTANGAZA MAFANIKIO YAKE KATIKA MPANGO WAKE WA NYUKLIA.

 TEHRAN-IRAN,

Rais wa Iran Ahmadinejad amesema hivi karibuni nchi yake itatangaza mafanikio makubwa iliyoyapata katika mapango wake wa nyuklia.akihutubia makumi ya maelfuya watu   katika sherehe za kutimiza miaka 79 ya mapinduzi ya nchi Ahmedinedjad amesema katika siku zijazo dunia itashuhudia kutangazwa kwa tangazo muhimu la mafanikio ya Iran katika mradi wake wa Nyuklia bila kufafanua zaidi.

 Wafuasi wa Rais huyo wakiwa wamebeba bendera za Iran na picha za mwanamapinduzi na  kiongozi mkuu wa kidini Bw Ayatollah ali Khamenei walipaza sauti zao kwa maneno ya kuzilaani Israel na Marekani.
Naye kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh aliyekuwa moja wa waalikwa katika sherehe hizo amesema kamwe Hamas hawataitambua Israael kama taifa, kiongozi huyo amesema ingawa wapinzani wao wanawataka kuacha upinzani dhidi ya Israel na kutambua uvamizi wa Israel kamwe hawatofanya hivyo kama wawakilishi wa Wapalestina.

 Sherehe hizo  zilikuwa za kukumbuka mapinduzi ya serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani ya rais Sha Mahammad Reza Pahlavi yaliyotokeaa  Mnamo mwezi Februari 11, 1979 ambayo yalifuatiwa na Uundaji wa taifa la kiislamu chini ya Kiongozi Ayatollah Ruhollah Khomeini.

No comments:

Post a Comment