Sunday, February 5, 2012

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA- GHANA YAITOA TUNISIA, GABON HOI KWA MALI.





Wachezaji wa mali wakishangilia baada ya kuitoa Gabon kwa mikwaju ya Penati.
Andrew Ayew wa Ghana akichuana na mchezaji wa Tunisia


Mabingwa mara nne ya kombe la mataifa la Afrika timu ya Ghana leo wamefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuwafunga Tunisia jumla ya magoli 2-1 katika mchezo uliokuwa mkali na kushudia dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 kuisha timu hizo zikiwa katika sare ya 1-1.
Magoli ya ghana yalifungwa na John Mensah dak. 10 na Andrew Ayew Dk. 101 huku lile la Tunisia likifungwa na Saber Khelifa dak. 42.Katika mchezo huo Ghana ndio walioonekana kuutawala huku Tunisia wakiishia Kujilinda na kufanya mashambulizi machache langoni mwa Ghana.

Kwa matokeo hayo Ghana wanaenda nusu fainali kukutana na timu ya Zambia ambayo jana iliwatoa Sudan kwa jumla ya magoli 3-0.

katika Mchezo wa awali wa robo fainali Mali ilifanikiwa kuwabwaga wenyeji waliobakia na moja ya wababe wa michuano ya mwaka huu Gabon kwa changamoto za mikwaju ya Penati 5-4 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1-1 katika dakika 90 za kawaida magoli yakifungwa na Erick Mouloungui wa Gabon dak. ya 55 na Chek diabate kwa upande wa mali daak. 84.
Ilipofika kipindi cha penati Mali walifunga penati zao zote lakini bahati mbaya kwa nyota wa Gabon Aubameyang ambaye shuti lake liliokolewa na kipa Diakate wa mali kabla ya Keita kufunga penati ya mwisho iliyoyafukia matumaini ya Gabon kusonga mbele katika michuano hiyo, kwa matokea hayo Mali inakwenda kukutana na Ivory coast ambayo jana pia iliwatoa wenyeji wengine wa michuano hiyo Guinea Bissau.

No comments:

Post a Comment